JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA


TANZIA


MKUU wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Salvatory Mabeyo anasikitika kutangaza kifo cha Afisa Mkuu Brigedia Jenerali Abdallah Athman Mwemnjudi (Mstaafu), kilichotokea mchana wa tarehe 01 Februari, 2021 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo.


Marehemu alizaliwa tarehe 01 Julai, 1956 katika Kijiji cha Kibindu,, Kata ya Kibindu,, Tarafa ya Magamba, Wilaya ya Handeni, katika Mkoa wa Tanga. Alipata Elimu katika ngazi mbalimbali ikiwemo Human Resource Management and Development Tanzania mwaka 2003 na Masters in Security and Strategic Studies Tanzania mwaka 2014. 


Marehemu alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania tarehe 01 Januari, 1977. Alihudhuria kozi ya Afisa Mwanafunzi nchini Misri na kutunukiwa Kamisheni tarehe 06 Mei, 1982. Marehemu alipandishwa cheo kuwa Brigedia Jenerali tarehe 17 Septemba, 2012 kulingana na kozi za Kijeshi alizohudhuria katika utumishi wake. Marehemu alitumikia Jeshi kwa muda wa miaka 39 na miezi 6 hadi alipostaafu utumishi Jeshini kwa umri tarehe 30 Juni, 2017.


Brigedia Jenerali Abdallah Athman Mwemnjudi (Mstaafu) alitunukiwa Medali mbalimbali wakati wa utumishi wake ifuatavyo:- Vita, Miaka 20 ya JWTZ; Utumishi Mrefu Tanzania; Miaka 40 ya JWTZ; Utumishi Uliotukuka Tanzania; Miaka 50 ya JWTZ; Miaka 50 ya Muungano; Miaka 50 ya Uhuru na Nishani ya Comoro. 


Katika utumishi wake Jeshini, Marehemu aliwahi kushika madaraka mbalimbali yakiwemo Afisa Mnadhimu Makao Makuu ya Jeshi  mwaka 2000 hadi mwaka 2008 na Mkurugenzi wa Mafunzo Jeshi la Akiba Makao Makuu ya Jeshi mwaka 2014, madaraka aliyohudumu hadi anastaafu Jeshi kwa Umri tarehe 30 Juni, 2017.


Heshima za mwisho kwa marehemu zitatolewa Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo tarehe 03 Februari, 2021 kuanzia saa 03:00 asubuhi. Baada ya hapo Mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda Kijiji cha Kibindu, Wilaya ya Handeni, Mkoa wa Tanga tarehe 03 Februari 2021 na mazishi yatafanyika tarehe 04 Februari 2021.  Marehemu ameacha mke na watoto.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, Amina.


Imetolewa na

Kanali Juma Nkangaa Issa Sipe 

Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano

+255 739 448 787


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...