Na Abdullatif Yunus
Maadhimisho ya Sherehe za Maadhimisho ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM kwa Mkoa wa Kagera zimefanyika mwisho wa Wiki iliyopita katika Kata ya Kibanga Wilaya ya Muleba zikitawaliwa na shamra na shangwe mbalimbali.
Akitaja Sababu Kuu zilizopelekea kufanyika kwa Sherehe hizo Kata ya Kibanga, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa Kagera Ndg. Chonya Miraji Michael wakati wa salaam zake kwenye Sherehe hizo amenukuliwa akisema "..Sherehe Kama hizi zimewahi kufanyika Kibanga Miaka zaidi ya 15 iliyopita, kipindi hicho Diwani akitokana na CCM, na Sasa tumeamua kurudi baada ya kupatikana Tena kwa Diwani wa CCM.."
Aidha Ndg. Chonya ameongeza kuwa tumekuja kuazimisha Sherehe za Kuzaliwa CCM kwa sababu Kuu Tatu, ambazo zinatokana na Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Mwaka huu isemayo, CCM Imara, Serikali Imara na Madaraka Imara ya Wananchi, Kaulimbiu hiyo ikidadavuliwa vyema kupitia maamuzi ya Wnakibanga waliyoamua katika Uchaguzi Mkuu uliopita kwa kumchagua Rais, Mbunge na Diwani wa CCM.
Akisisitiza namna jinsi Chama kilivyofurahishwa na Ushindi huo wa Uchaguzi uliopita katika Kata hiyo ya Kibanga pamoja na maeneo mengine, Mgeni Rasmi katika Sherehe hizo ambae pia ni MNEC wa Mkoa Kagera Ndg. Willbroad Mutabuzi mbali na shukrani zake kwa Uongozi wa Mkoa chini ya Brigedia Marco Gaguti kwa usimamizi mzuri wa Shughuli za Serikali Mkoani Kagera, ameongeza kuwa kwa Sasa Chama Kitakuwa Imara zaidi kusimamia Serikali hasa katika utekelezaji wa Miradi ikiwa sambamba na kulinda miundombinu isiharibiwe na kuhujumiwa.
Ndg. Mutabuzi katika kujibu moja ya Kero za kipindi kirefu ambayo Ni Barabara ya Kibanga Mbunda ambayo imekuwa korofi kwa kipindi kirefu Sasa, amekiri kujionea Barabara hiyo na kuwahakikishia Barabara Hiyo itajengwa kwani Taarifa aliyopewa na Meneja wa TARURA Mkoa Kagera ni kwamba tayari mkandarasi amekwishatafutwa na Muda wowote atakuwa kazini.
Mgeni na Rasmi na Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa (NEC) Komredi Willbroad Mutabuzi akizungumza na Wananchi wakati wa Sherehe za Kuzaliwa kwa CCM Mkoa Kagera Zilizofanyika Kimkoa Kata Kibanga Wilaya ya Muleba.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Muleba Ndg. Athuman Kahara akizungumza wakati wa Sherehe za Kuzaliwa kwa CCM Mkoa Kagera Zilizofanyika Kimkoa Kata Kibanga Wilaya ya Muleba.
Muonekano wa Keki iliyokatwa kusherehekea Sherehe za Kuzaliwa kwa CCM Mkoa Kagera Zilizofanyika Kimkoa Kata Kibanga Wilaya ya Muleba.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana (UVCCM) Mkoa Kagera Happiness Kashunju Lunyogote akikata kata vipande vya keki Mara baada ya kukatwa keki hiyo Maalum tayari kwa kuliwa, pembeni Ni Ndg. Chonya Katibu wa CCM Kagera.
Katibu wa CCM Wilaya ya Bukoba Vijijini Komredi Paulo Mwita, akisambaza Vipande Vya Keki kwa Watoto ishara ya kushiriki furaha pamoja na Watoto hao waliohudhuria Sherehe za CCM Wilayani Muleba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...