
WAFANYAKAZI wanaofanya kazi ya kukagua mizigo na bidhaa mbali mbali za wageni wa ndani na nje ambao wako kwenye kozi ya kitaifa ya ukaguzi wa mizigo kwa kutumia mionzi inayondeshwa na Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) yenye makao makuu yake jijini Arusha, jana wamefanya mafuzo hayo kwa vitendo katika maeneo ya viwanja vya ndege, maabara za Tume na katika hoteli.
Mratibu wa mafunzo hayo wa Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC) Atumaini Makoba amesema mafunzo kwa vitendo yanasaidia maeneo ambayo mionzi inapotoka kwenye mashine za ukaguzi wa mizigo ili waweze kupunguza wingo wa mionzi wanayopata pasipo lazima kwa kukosa maarifa ya mahala pazuri pa kufanya kazi zao ili kujilinda madhara yanayoweza kujitokeza wakati wanafanya kazi zao.
“Hapa sasa tunawaonesha yale waliyosoma darasani kwa vitendo ili kuwapa ujuzi zaidi kwani itawasaidia kuepukana na madhara ya mionzi maana lazima anayepima mizigo afahamu kwa kina wapi mionzi inapotokea na inapoelekea wakati akifanya kazi hiyo”alisema Makoba wakati wa mafunzo hayo kwa vitendo.
Amesema katika kujifunza kwa vitendo ameona wapo baadhi ya wafanyakazi waliokuwa wakikosea katika utendaji wao wa kila siku, lakini baada ya kuwaonesha kwa vitendo wameweza kurekebisha pale walipokuwa wakifanya tofauti na kwamba sasa wana uhakika wataendelea kuzingatia usalama wa mionzi kwenye maeneo yao ya kazi ili kujilinda na kuilinda jamii kwa ujumla.
Kwa upande wake kiongozi wa maofisa hao waliohudhuria mafunzo kwa vitendo Bwana Lusajo Masosi amesema mafunzo hayo ya vitendo yamewejengea uwezo wa namna ya kujilinda na athari za mionzi katika maeneo yao ya kazi.
Jumla ya maofisa 40 kutoka katika maeneo ya ujenzi wa miundombinu kama barabara na mamlaka mbalimbali kama vile viwanja vya ndege, hotelini, viwandani na bandarini wanashiriki mafunzo hayo ya matumizi salama ya teknolojia ya mionzi kwa siku tano hapa makao makuu ya TAEC-Arusha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...