Raisa Said,Tanga.


Ile changamoto ya Wazazi kuwaficha watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi  Mkoani Tanga  imepungua baada ya elimu kutolewa kwa jamii.

Akizungumza na Waandishi wa habari Katika kituo cha  kulelea watoto wenye ulemavu kilichopo Jijini Tanga (YDCP) Mtoa tiba kwa vitendo  Emanuel Mnyone alisema  wazazi wengi wamekuwa na mwitikio mkubwa wa kuwapeleka watoto Katika kliniki ilipo kituoni hapo tofauti na zamani.

" Kwasasa  Wazazi wengi wamekuwa na msukumo mkubwa wa kuwafikisha watoto kituoni kwetu kwaajili ya kliniki na kufanya mazoezi tofauti na ilivokuwa siku za nyuma" Alisema Mratibu huyo

Mtoa tiba  huyo alitumia fursa hiyo kuwashauri wanawake walio katika umri wa kuzaa kutumia vyakula vyenye Madini ya folic acid ili kuepuka kuzaa watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi.

Alisisitiza kuwa ulaji wa mboga za majani pamoja na matunda kwa wingi husaidia kuzalisha Madini hayo kwa wingi ambayo yanasaidia kuwa ni kinga kwa mwanamke huyo.

 Anaendelea kusema kuwa kuwa iwapo Madini hayo yatakuwepo ya kutosha katika mwili wa mama mjamzito Kuna uwezekano wa zaidi ya asilimia 90%kuzaliwa kwa mtoto wenye Afya Bora.

Kuhusu wasichana ambao wapo kwenye umri wa kubeba mimba amewashauri vyakula hivyo alivyoainisha na dawa za folic acid kabla ya ujauzito na miezi mitatu ya ujauzito ili kusaidia kuzaa watoto wenye Afya Bora.

Amina Omary Mkazi wa Kasera Jijini Tanga alisema wazazi wengi wanapojifungua mtoto mwenye matatizo  kama hayo ikiwemo ulemavu wa viungo wamekuwa wanawaficha wakiamoni kuwa ni mambo ya ushirikina lakini kwa sasa elimu inayotolewa na watalaam wa afya imewafanya waanza kuwafichua na kufuata mashart wanayopewa.

" Ushauri tunaopewa na wataalam wa afya kuhusu vyakula umetufanya tubadilike na kufuata mashariti ikiwemo kwenda kliniki bila kuogopa tofauti na siku za nyuma " Alisisistiza  Mama huyo .

Hivi karibuni Mjumbe wa Chama  cha Wazazi wenye watoto wenye vkichwa kikubwa na mgongo wazo , Mkoa wa Tanga, Oscar Changala alisema kuwa  kumekuwa na changamoto ya kupata  takwimu  ya  watoto wenye vichwa vikubwa  kutokana  na wazazi  wengi  wengi kuwaficha  watoto  hao .



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...