Charles James, Michuzi TV

Rais Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dk Jakaya Kikwete leo walipokutana katika kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi leo.

Katika kikao hicho ajenda mbili zilijadiliwa ambapo mojawapo ni ushiriki wa Chama hicho kwenye msiba wa aliyekua Rais Dk John Magufuli ambaye pia alikua Mwenyekiti wa CCM.

Ajenda ya pili ni kuitisha kwa haraka kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho ya kuchagua Mwenyekiti wa Chama hicho.

Kwa mujibu wa Katibu wa Itikadi na Uenezi ya CCM, Humphrey Polepole amesema kama ilivyo desturi ya chama hicho wataenda kupendekeza jina moja tu la Rais Mama Samia Suluhu Hassan kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho.

Hayo yamejiri kufuatia kifo cha Rais na Mwenyekiti wa CCM Dk John Magufuli kilichotokea Machi 17 mwaka huu katika Hospitali ya Mzena alipokua amelazwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo.

Hayati Dk Magufuli atazikwa Machi 26 wilayani Chato mkoani Geita baada ya shughuli za kuagwa kufanyika katika Mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma atakapoagwa kitaifa kisha kuagwa Zanzibar na Mwanza na baadae Chato.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...