Charles James, Michuzi TV

TUNALIA! Hii ni kauli ya Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania Wilaya Dodoma Mjini (UWT), Diana Madukwa kufuatia kifo cha Rais Dk John Magufuli ambaye pia alikua Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM.

Akizungumza na Michuzi Blog jijini Dodoma, Diana Madukwa amesema moyo wa uzalendo na kulipenda Taifa lake ndio kulimfanya Rais Dk John Magufuli kuwatumikia watanzania kwa wivu na upendo mkubwa huku akiyatanguliza mbele maslahi ya watanzania.

Amesema Taifa kwa ujumla halina budi kumlilia na kumuombea Dk Magufuli kwani ndani ya kipindi kifupi cha miaka mitano amefanya mambo makubwa akigusa kila sekta.

Amesema yeye kama kiongozi anaetokana na Umoja huo wa Wanawake anamshukuru Mungu kwa zawadi ya Rais Magufuli ambaye pia kwenye serikali yake aliwaamini wanawake na kuwapa kipaumbele katika nafasi mbalimbali hata zile nyeti na zilizokua zikionekana kuwa ni ngumu kwa Mwanamke.

" Aliyagusa maisha yetu kwa mambo makubwa aliyoyafanya kwenye Nchi yetu hasa wanyonge, alitutetea na kutuheshimisha hata Mataifa makubwa yakatujua na kutuheshimu.

Ni Rais ambaye ameimarisha uchumi wa Nchi na leo kupitia yeye tumefikia uchumi wa kati, ameimarisha miundombinu yetu kuanzia barabara, anga na hata majini ni wazi Taifa limepoteza Baba, Kiongozi na Mzalendo aliyeipenda Nchi yake na watanzania wenzake," Amesema Diana Madukwa.

Amesema wao kama UWT Wilaya ya Dodoma Mjini wataendelea kuyaenzi na kuyafuata yale yote mazuri ambayo yamefanywa na Rais Dk John Magufuli kwa kipindi chote cha uongozi wake.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...