Mabalozi
wanaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nje ya Nchi
wameelekezwa kujipanga, kushiriki na kutafuta fursa zitakazowezesha
bidhaa mbalimbali za Tanzania kupata masoko ya uhakika katika nchi
walizopo.
Agizo
hilo limetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi wakati akizungumza na mabalozi
wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi na kuongeza kuwa , Ilani ya Chama
cha Mapinduzi inatamka bayana juu ya diplomasia ya uchumi sambamba na
kuimarisha sauti ya Tanzania na taswira yake katika medani ya uhusiano
wa kikanda na kimataifa.
Prof.
Kabudi ameongeza kuwa ili kufanikisha hilo Balozi zinapaswa kuimarisha
ushiriki wa Tanzania katika jumuiya nyingine za kimataifa zikiwemo,
Indian Ocean Rim Association, Indian Ocean Tuna Commission, South South
Commission, South West Indian Ocean Fisheries Commission.
Aidha
amewataka Mabalozi hao kuzingatia maelekezo ya Mheshimiwa Dkt. Hussein
Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
aliyoyatoa wakati akizundua Baraza la Wawakilishi ya kutaka Uchumi wa
Bluu kupitia uvuvi wa Bahari Kuu unakuwa na manufaa kwa Wananchi
hususani katika kuongeza mapato, ajira na kukuza uchumi kwa kuzingatia
kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni ya
Muungano.
Pia
Prof. Kabudi amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango unaotolewa
na Watanzania waishio nje ya nchi (Diaspora) katika maendeleo ya Taifa
na kuzielekeza Balozi zianze na ziboreshe kanzi data ya Diapora ikiwa
ni pamoja na kuwahimiza kuanzisha Jumuiya zao.
“Natambua
kazi hiyo inaendelea na kwa sasa tuna data za diaspora takriban 98,658
na kuna jumuiya 77 za diaspora. Nichukue fursa kusisitiza umuhimu wa
Balozi zetu kuboresha na kuharakisha zoezi hili kwa kubuni njia
mbalimbali za kuwaandikisha”. Amesema Prof. Kabudi
Mkutano
huo wa Prof. Palamagamba John Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje
ya nchi umehudhuriwa pia na Naibu Waziri, Mhe William Tate Ole Nasha,
Katibu Mkuu Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, Wakurugenzi na Wakuu wa
Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki.
Sehemu
nyingine ya Mabalozi na Wakuu wa Idara na Vitengo wakifuatilia hotuba
ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof.
Palagamba John Kabudi (Mb) kwenye Kikao Kazi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...