MAHAKAMA ya Mwanzo Buguruni, Dar es Salaam, imevunja ndoa Magreth Silaeli (37) na mume wake, Raymond Kulaya (44) baada ya kujiridhisha kuwa ndoa hiyo imeshindwa kurekebishika kufuatia kuishi mbali mbali kwa miaka 10.

Ndoa hiyo imevunjwa chini ya kifungu cha 107 (2) (f) cha sheria ya ndoa na mahakama imepewa Mamlaka ya kufanya hivyo chini ya kifungu cha 110 cha sheria hiyo ya ndoa.

Aidha,  Silaeli ambaye ndio mdai katika kesi hiyo talaka namba 82 ya mwaka huu, ameieleza mahakama kuwa yeye na mzazi mwenzake wa sasa, wanatarajia kufunga ndoa Novemba mwaka huu jambo ambalo liliungwa mkono na mdaiwa ambaye ameeleza kushirikiana naye kufanikisha ndoa hiyo mpya.

Katika hukumu hiyo iliyosomwa na Hakimu Matrona Luanda leo Machi 17, 2021 imeeleza kuwa, licha ya ndoa hiyo kipitia kwenye baraza la usuluhishi lakini ilishindikana  kurekebishika.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Luanda  Silaeli (mdai) aliieleza mahakama kuwa alifunga ndoa na Kulaya Machi 18, 2006 lakini hawakubarikiwa kupata watoto na wala kuchuma mali yoyote pamoja isipokuwa mdaiwa Kulaya) alikasirishwa na kitendo cha wao kutopata watoto n ku wa apelekea kufikia uamuzi wa kutengana, mwaka 2011.

Baada ya kutengana, Silaeli alipata mwanaume mwingine na kufanikiwa kuzaa naye watoto wanne huku mwanaume akipata watoto watatu na mwanamke mwingine.

Amesema kufuati hayo, Silaeli alifika mahakamani na kuomba talaka kwa sababu hawaishi pamoja na mdaiwa kwa zaidi ya miaka 10.

"Mdaiwa alipoitwa aliieleza mahakama kuwa ni kweli walifunga ndoa ya kikristu mwaka 2006 lakini walifikia uamuzi wa kutengana ili kila mmoja akatafute watoto," amesema Hakimu Luanda.

"Baada ya mahakama kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili ilijiuliza maswali matatu, je mdai na mdaiwa walioana kwa ndoa, je, ndoa imevunjika na imeshindwa kurekebishika na nani mshindi katika shauri hilo?

Ameeleza ushahidi unaonyesha kuwa ni kweli mdai na mdaiwa walifunga ndoa ya kikristo Machi 18,2006 lakini hawakuishi pamoja kwa miaka 10 huku kila mmoja akiishi kwake licha ya baraza la usuluhishi kujaribu kurekebisha ndo hiyo bila ya mafanikio

"Nimeridhika na maelezo ya mdai na ndio ameibuka mshindi katika shauri hili na kwa Mamlaka niliyonayo ndoa hii imevunjwa hivyo, mdai apate talaka yake ndani ya siku 45 na haki ya rufaa kwa asiyeridhika ipo wazi." Amesema Luanda.

Akizungumza nje ya mahakama, Silaeli amesema waliishi kwa miaka mdaiwa kwa mitano bila kupata watoto na kwa sababu matamanio yao yalikuwa ni kupata watoto waliamua watengane mpaka sasa ambapo ameamua kuja ahakamani kudai talaka ili kila mmoja abariki ndoa yake maana kila mmoja anafamilia yake.

"Nimefurahia hukumu hii, Novemba Mwaka huu  natarajia kubariki ndoa yangu na mtu ambaye naishi naye sasa ili tuishi maisha ya kumpendeza Mungu kama mahakama ingeamua vinginevyo tungevumilia mpaka mwakani," amesema Silaeli.

Ameongeza kuwa,  yeye na aliyekuwa mume wake hawana tatizo lolote kwani wanaishi vizuri na wanaendelea kuwasiliana kama marafiki wa kawaida.

Kwa upande wake,  Kulaya amesema hakuna mtu aliyewahi kuwaingilia katika ndoa yao kuuliza kwa nini hawapati mtoto, walikaa wenyewe na kuamua kila mmoja akatafute mtoto ili kuepusha kugombana endapo  mmoja wapo angepeleka  mtoto wa nje ya ndoa yao.

"Tunaishi kwa amani, mwenzangu amejaliwa watoto wanne na mimi ninao watoto watatu na kabla ya ndoa nilikuwa nao wawili. Nimekubaliana na maamuzi ya mahakama wote tumeshinda katika kesi hii hatukuwa na mali hivyo, tusingweza kugawana vyumba vya kupanga" amesema.

Aliongeza wangeweza kusubiri huenda Mungu angewapatia zawadi hiyo ya watoto lakini ndiye anayejua na tayari yameshatokea hivyo, hawezi kumnyang'anya mwanaume mwenzake watoto wake eti kwa sababu amelima kwenye shamba lake.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...