Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt. Aggrey Mlimuka amesema Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa Tatu wa Wanawake katika Uongozi utakaoambatana na Mahafali ya Nne, Tano na Sita ya Programu ya Mwanamke Kiongozi.

Mkutano Mkuu wa Tatu wa Wanawake katika uongozi na mahafali hayo yanatarajia kufanyika kesho Mkoani Dar es Salaam ikihudhuriwa na viongozi wengine mbalimbali.

Dkt Mlimuka amesema kwamba mkutano wa mwaka huu umebeba ujumbe unaosema “Ukuzaji wa Vipawa vya Wanawake Walio Katika Uongozi ili Kuwa na Mashirika Endelevu” lengo likiwa ni kuwaleta pamoja viongozi wa makampuni, mashirika binafsi, mashirika ya umma, mashirika ya kimataifa, taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa wakiwemo Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini pamoja.

Amesema, kukutana pamoja na wadau wote wa uongozi lengo ni kujadili namna nzuri ya ujumuishwaji wanawake kwenye nafasi za juu za uongozi kwa Kubadilishana ujuzi na uzoefu kuhusiana na ujumuishwaji wa wanawake katika nafasi za juu za Uongozi wa Makampuni na Taasisi za Kibiashara.

Dkt Mlimuka ameeleza malengo mengine ni Kushuhudia na kusherekea mafanikio mbalimbali yaliyotokana na Programu ya Mwanamke Kiongozi tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 2016, Kujadili changamoto na fursa zinazohusiana na mwanamke katika uongozi na namna ya kuzikabili na Kuongeza ufahamu kuhusiana na faida za kuwa na usawa wa jinsia katika maeneo ya kazi.

Aidha amesema, Mkutano huo itahusisha pia katika Kusisitiza umuhimu wa Ushirikishwaji wa wanaume katika maeneo ya kazi ili kuongeza uwezeshwaji wa wanawake kiuchumi,Kubadilishana uelewa na uzoefu kuhusiana na uhitaji wa kuwashirikisha wanawake katika uchumi wa kidijitali na Kubadilishana uelewa na uzoefu katika ujumuishwaji wa wanawake katika nafasi za juu za uongozi katika maeneo ya kazi.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt Aggrey Mlimuka akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Mkutano Mkuu wa 3 wa Wanawake katika Uongozi utakaoambatana na Mahafali ya 4, 5 na 6 ya Programu ya MWANAMKE KIONGOZI utakaofanyika kesho Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...