Mkuu wa Wilaya ya Karatu Abbas kayanda akiwa Katika stoo ya dawa ya zahanati ya Ayalabe iliopo Katika tarafa ya Karatu Wilayani humo mkoani Arusha alipo fanya ziara ya kikazi juzi(picha na Woinde Shizza , ARUSHA)

Na Woinde Shizza , michuzi Tv - ARUSHA
TATIZO la watumishi wa afya kutokuwa na rejista ya madawa yanayoingia na kutoka katika vituo vya afya imesababisha upotevu wa dawa za serikali.

Hali hiyo imeongeza mwanya wa dawa za serikali kupotea au kuchelewa kuagizwa kwa sababu ya kukosa takwimu sahihi ya kiasi cha dawa zilizoisha na takwimu ya dawa zinazohitajika katika vituo vya huduma ya afya vilivyoko wilayani Karatu mkoani Arusha.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Abbas Kayanda alipofanya ziara
katika zahanati ya Ayalabe na Tloma iliopo tarafa ya Karatu ambapo katika ziara hiyo amefanya ukaguzi wa store za dawa katika zahanati hizo ili kujiridhisha kama dawa zilizopo zinaendana na mahitaji ya kituo.

Kayanda alimtaka Mkaguzi wa ndani na Mganga mkuu wa wilaya kufanya ukaguzi wa vituo vyote vya afya ili kujua hali ya upatikanaji wa dawa, na ubadhidhilifu wowote utakaoonekana, wahusika warejeshe na hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yao.

Alisema utaratibu wa kukagua dawa katika vituo vya kutolea huduma ya afya utakuwa unafanyika kila baada ya miezi mitatu ili kupata takwimu sahihi za dawa zinazoagizwa MSD na dawa zilizopo katika vituo vya afya.

Kayanda alitoa onyo kwa baadhi ya wahudumu wa afya wasio waaadilifu katika kituo cha afya Karatu wenye tabia za kuwaelekeza wagonjwa kununua dawa katika maduka ya watu binafsi kuacha mara moja kwani akibainika hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake.

"Mtumishi yeyote atakayebainika kumuelekeza mgonjwa kununua dawa kwenye maduka binafsi, vitendo hivyo vinaenda kinyume na sera ya serikali ya kuboresha huduma za afya na upatikanaji wa dawa katika vituo vyote vya afya ili wananchi waweze kupata mahitaji yote ya kitabibu katika vituo vya afya vya serikali, lakini pia kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya afya iliyoboreshwa inayowezesha kituo cha afya kuwa na uwezo wa kununua madawa kwa kujitegemea kulingana na mahitaji."Alisema

Katika hatua nyingine Kayanda ameelekeza kuandaliwa kwa utaratibu maalumu wa kuwajulisha wakinamama wenye watoto wadogo kuja kwa pamoja kupata chanjo ya polio kwa watoto wao badala ya utaratibu wa kuwaacha kuhudhuria kliniki kwa uchache kwa ajili ya kupata chanjo ya polio , ambapo alibainisha kuwa chupa moja chanjo inahitaji kutumika kwa watu 17 hivyo kufungua chupa kwa watu wachache ni kuharibu chanjo hizo.

Aidha alitoa maelekezo kwa mganga mkuu wa wilaya ya Karatu kushughulikia swala la malipo ya walinzi katika zahanati ya Ayalabe na Tloma waliokuwa wanadai malikimbizo ya mishahara , ikiwa nipamoja na kuandaa utaratibu wa kuwaweka kwenye bajeti ili kuondoa matatizo ya malimbikizo ya madeni inayojitokeza mara kwa mara katika zahanati hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...