KAMANDA Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilbroad Mutafungwa amesema kuwa madereva wanatakiwa kujiepusha na ajali ambazo kuepukana huko kunatokana na kufuata sheria za usalama Barabarani.

Mutafungwa ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na madereva kituo cha Mabasi cha Magufuli Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam amesema kuwa madereva hawahitaji mashindano kwani wakitoka katika kituoni hapo wanakuwa wanapofika katika vituo wanakuta Abiria walishakata tiketi.

Amesema kuwa ajali zinagharimi uchumi wa nchi kutokana na watu wa hao ni nguvu kazi ya taifa lakinin pia wanawategemezi wao.

Kamanda Mutafungwa amesema kuwa dereva wakati wa kusafiri anakuwa na posho hivyo anatakiwa posho yake ale na familia yake ikitokea anavunja sheria posho yake hiyo itakwenda serikalini kwani hakuna mmiliki anayeweza kulipa Makosa ya dereva mzembe.

Aidha amesema kuwa katika kipindi cha sikukuu ya pasaka madereva wanakumbushwa kuendelea kuzingatia sheria za usalama Barabarani ili wananchi washerekee siku kuu bila majozi.

Amesema madereva watakwenda tofauti na sheria watapigwa faini zitawahusu.

Mutafungwa amesema kuwa abiria wanatakiwa kuwa na uhakika na safari zao na sio kuwa na mashaka na madereva kwa wale wenye kazi ya kudhibiti tutashughulika nao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...