KAIMU Kabidhi Wasii Mkuu wa Wakala wa Usajili , Ufilisi na Udhamini (RITA,) Bi.Emmy Hudson hii leo Jijini Dodoma amewasilisha taarifa kwa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu utekelezaji wa mkakati wa Taifa wa Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu na Takwimu Tanzania Bara.
Mkakati huo umelenga kuangalia masuala ya Mfumo wa Usajili, kupitia Sheria ya Usajili, kuboresha Mfumo wa TEHAMA na kuimarisha mahusiano baina ya Taasisi zinazohusika na majukumu ya usajili.
"Huu Mkakati ni wa Kitaifa na unajibu matakwa na kuboresha hali ya Usajili wa Vizazi na Vifo na upatikanaji wa uhakika wa takwimu za matukio muhimu ya binadamu na kuwezesha Serikali kuimarisha mifumo yake ya maendeleo katika nyanja za uchumi, jamii,Siasa, ulinzi na usalama." Alisema Bi.Hudson.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...