Charles James, Michuzi TV
SPIKA wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema kuwa kufuatia kifo cha Rais Dk John Magufuli Watanzania wanakazi ya kuhakikisha wanaendeleza yale ambayo Raisi Magufuli alikuwa akiyafanya.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma leo, Job Ndugai amesema Rais Magufuli alikua mjenga nchi hasa katika suala zima la miundombinu na miradi mikubwa mingi kama elimu, afya na barabara nakusema kuwa ameacha alama kwenye kila nyanja.
Amesema kuwa kazi zote alizokuwa akizifanya Raisi Magufuli na hotuba alizozitoa bungeni sambamba na utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2020/25 zitasimamiwa na kutekelezwa.
Aidha ameagiza Wabunge wote waliokuwa kwenye ziara ya kukagua miradi ya maendeleo kwenye kamati zao warudi haraka na mpaka sasa wabunge wote wako njiani kurudi dodoma.
Sambamba na hayo amesema Rais alikuwa muhimili wa pili wa Bunge hivyo ni pigo kwa Bunge na amemuachia kazi kubwa Makamu wa Rais Mama Samia na viongozi wote na serikali kwa ujumla huku akitoa pole kwa Mke wa Rais Magufuli, Mama Janeth Magufuli, Familia yake na watu wa Chato na kwa Watanzania wote.
Home
BUNGENI
SPIKA NDUGAI AMLILIA RAIS MAGUFULI, AAGIZA WABUNGE WOTE KUSITISHA ZIARA ZA KAMATI NA KUREJEA DODOMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...