Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania ( TFF) limesema kuwa mchezo wa makundi kufuzu Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) dhidi ya Libya hautakuwa na mashabiki..

Taarifa iliyotolewa na TFF, imesema kuwa mchezo huo utakaochezwa Machi 28 dhidi ya Libya hautakuwa na  mashabiki baada ya kupokea barua kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Mchezo kati ya Taifa Stars na Libya utapigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kuanzia sa 10  alasiri

TFF wamesema kuwa, wamepokea maelekezo kutoka CAF kuwa katika mchezo huo hautakuwa na mashabiki.

Mbali na hilo, Timu ya Taifa nashuka dimbani usiku huu kuwakabili timu ya Taifa ya Equatorial Guinea katika mchezo wa makundi kufuzu Fainali za Mataifa Ya Afrika (AFCON).

Mchezo hyo unaotarajiwa kupigwa saa 4 ya usiku kwa masaa ya Afrika Mashariki utapigwa katika nchi ya Equatorial Guinea.

Baada ya kukamilika kwa mchezo huo  Taifa Stars watarejea nchini kwan ndege ya kukodi ili kujiandaa na mchezo wa Jumapili dhidi ya Libya.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...