Emmanuel Bundala (aliyevaa koti jekundu) akiungana na watoto wanaoishi mitaani kula chakula cha mchana kilichoandaliwa na Kanisa la Pentekoste la PHAMT Bethania Dodoma kwenye viwanja vya Nyerere Square. Emmanuel ni mtoto wa Askofu Bundala ambaye alishiriki kuwatakusanya watoto hao pamoja maandalizi ya chakula hicho. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

Askofu Julius Bundala wa Kanisa la Pentekoste la PHAMT Bethenia Dodoma akiwahubiria watoto wanaoishi mitaani baada la kula nao chakula cha mchana siku ya Jumatatu ya Pasaka kwenye viwanja vya Julius Nyerere jijini Dodoma.

Watoto wanaoishi mitaani wakinawishwa mikono tayari kupata chakula


Wakigawiwa chakula

Sasa ni wakati wa kula








Mtoto anayeishi mitaani Joseph Jailos(17) akielezea jinsi alivyotoka Kigoma hadi kwenda Dodoma ambako hadi sasa anaishi mitaani.

Mtoto anayeishi mitaani Godfrey John Bosco (15) aliyeishia darasa nne katika Shule ya Msingi Majengo mkoani Kigoma, akielezea jinsi alivyotoka Kigoma hadi kwenda Dodoma ambako hadi sasa anaishi mitaani.
Mtoto anayeishi mitaani, aliyejulikana kwa jina la Athuman kutoka mkoani Kigoma, akielezea mahasibu mbalimbali wanayopata wanapotafuta riziki mitaani.
Emmanuel Bundala mtoto wa Askofu Julius Bundala wa Kanisa hilo, akielezea lengo la kuwaandalia chakula watoto hao. Kwa habari zaidi sikiliza kupitia clip ya video hapo chini..
Askofu Bundala (kulia) akiwa na baadhi ya watoto wanaoishi mitaani pamoja na familia yake baada ya kupata mlo.

Na Richard Mwaikenda, Dodoma
Askofu Julius Bundala wa Kanisa la Pentekoste la PHAMT Bethenia Dodoma akiwahubiria watoto wanaoishi mitaani baada ya kula nao chakula cha mchana siku ya Jumatatu ya Pasaka kwenye viwanja vya Julius Nyerere jijini Dodoma. Baada chakula aliwahubiria kwa kuwataka kumrudia Yesu Kristo ili warudi kwenye hali yao ya kawaida badala ya kuishi maisha yasiyofaa mitaani. 

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza/kuona kupitia clip hii ya video, Askofu Bundala, mwanaye Emmanuel wakielezea lengo la kuwasaka watoto hao na kula nao chakula pamoja na kuwahubiria neno la Mungu lakini pia utawasikiliza watoto wakielezea pamoja na mambo mengine na jinsi wanavyopatwa na maswahibu wanapoishi mitaani....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...