Na Amiri Kilagalila,Njombe
Baraza
la wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoa wa
Njombe wametoa wito kwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia
Suluhu Hassan kuingilia kati ili kuondolewa kwa wabunge 19 wa viti
maalum wanaodaiwa kuwa ni wabunge waliotokana na Chama hicho ili hali
wamefukuzwa uanachama.
Wito huo umetolewa na baraza hilo wakati wakizungumza na vyombo vya habari katika mkutano wao uliofanyika mkoani hapo.
Siglada
Mligo ni katibu wa BAWACHA mkoa wa Njombe amesema Rais ana mamlaka yote
kisheria kuingilia kati mhimili wowote unapokwenda kinyume na sheria
hivyo anaamini anaweza kulishughulikia swala hilo la wabunge 19
wanaodaiwa kuto kuwa na vyama huku wakiendelea kutia doa demokrasia na
utii wa sheria.
“Rais kwa
mujibu wa katiba ana mamlaka ya moja kwa moja kuingilia mhimili wowote
pale unapokwenda kinyume na sheria,kwa hiyo ana uwezo mkubwa wa kutoa
amri pale atakapojiridhisha wale wabunge 19 wapo pale kinyume cha sheria
na katiba,naamini anaweza kushughulika nao kwasababu amekuja kwa mpango
wa Mungu” aliesema Siglada Mligo
Amesema
anashangazwa kuona kiti cha spika kinaendelea kuwalinda wabunge hao ili
hali mwaka 2017 walio kuwa wabunge wengine akiwemo Sophia Simba (CCM)
alifukuzwa uanachama na ubunge ukakoma lakini pia mwaka huo huo wabunge
viti maalum 8 walifukuzwa uanachama na Chama Cha CUF chini ya mwenyekiti
wao Lipumba na ubunge wao ukakoma,inakuwaje wabunge hao 19 waliofukuzwa
uanachama wa Chadema kushindikana kupndolewa bungeni.
“Mwaka
2017 kuna mbunge wa CCM Sophia Simba alifukuzwa na Chama chake na Spika
wa Bunge Jobu Ndugai alitoa taarifa bungeni na ubunge wake
ukakoma.Lakini ilivyokuja kwa CHADEMA kuwafukuza uanachama wanachama
19,spika wa bunge huyo huyo ameahidi kuwalinda”Siglada Mligo katibu wa
BAWACHA mkoa wa Njombe
Jeni
Mgeni ni mwenyekiti wa baraza la wanawake wa chama hicho wilaya ya
Njombe na Levina Wikechi ni mwenyekiti wa baraza la wanawake wa chama
hicho kata ya Ramadahani,wanasema wao hawawatambui wabunge hao huku
wakimuoba Rais kuondosha wabunge hao ili kuimarisha uongozi wake.
“Sisi
tunazidi kujiuliza hivi Ndugai yuko pale kwasababu gani na hatuwezi
kuamini anavyooendelea kukaa nao pale bungeni na anaahidi kuwalinda
kabisa,tunaomba Rais askie kilio cha sisi wanawake wenzake ambao
hatupendi kuona katiba inavunjawa wazi”alisema na Levina Wikechi
Naye
Jeni Mgeni amesema “Kutokana na matamkoa ya Rais wa sasa ninaamini
demokrasia itakaa vizuri na hawa wabunge walioenda bila utaratibu wa
Chama naamini anaweza akaliweka sawa.Na sisi tunachokitaka zaidi kwa
Rais wetu tuanomba kwanza tume huru lakini pia mabadiliko ya
katiba”alisema Jeni Mgeni
Aidha
wameeleza kuwa Chama hicho bado kipo imara na kinaendelea na shughuli
zake huku wakitoa rai kwa wanachama kuendelea kuwa wavumilivu na
kusikiliza viongozi wao wanasema nini.
Walengwa
ni Halima Mdee, Esther Matiko, Grace Tendega, Cecilia Pareso, Ester
Bulaya, Agnesta Lambart, Nusrati Hanje, Jesca Kishoa, Hawa Mwaifunga,
Tunza Malapo, Asia Mohammed, Felister Njau, Nagenjwa Kaboyoka, Sophia
Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Fiao, Anatropia Theonest, Salome
Makamba na Conchesta Rwamlaza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...