Na Mwandishi wetu, Babati
MKURUGENZI
wa kampuni ya Farm Green Imprements LTD, Dunga Othman amefikishwa
Mahakamani na kushtakiwa kwa kujipatia fedha shilingi milioni 58.4 kwa
njia ya udanganyifu kuwa atawapa matrekta wakulima watatu wa Wilaya ya
Hanang' ahadi ambayo hakuitekeleza.
Mkuu
wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoani Manyara,
Holle Joseph Makungu amesema Dunga alikamatwa Tuangoma Dar es salaam na
kusafirishwa hadi mjini Babati, kuweza kukabiliana na mashtaka yake
katika kesi namba CC.1/2021 inayohusu kujipatia fedha kwa njia ya
udanganyifu.
Makungu
amesema Dunga amesomewa mashtaka yake na wakili wa TAKUKURU Martin
Makani katika mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Manyara Simon Kobelo.
Amesema
Dunga amesomewa mashtaka matatu ya kujipatia fedha shilingi milioni
58.4 toka kwa wananchi watatu wa Wilaya ya Hanang' kwa udanganyifu kuwa
atawaletea matrekta ahadi ambayo hakuitekeleza tangu mwaka 2016.
"Uchunguzi
wetu umebaini kuwa Dunga alijipatia fedha hizo kupitia kampuni ya Farm
Green Imprements LTD kwa ahadi ya kuwaletea matrekta wananchi hao,"
amesema Makungu.
Amesema
hata hivyo, Dunga hakuwaletea wananchi hao matrekta wala kurejesha
fedha, zaidi akaua kampuni ya Farm Green Imprements LTD aliyoitumia
kujipatia fedha na kuanzisha kampuni nyingine iitwayo PLANCON (T) LTD.
Amesema
baada ya kusomewa mashtaka yake Dunga ameyakana na mahakama ilimpa
masharti ya dhamana ambayo ni kuwasilisha Mahakamani fedha taslimu
shilingi milioni 29.1 au mali yenye thamani ya shilingi milioni 58.4.
"Aidha
ametakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao watamdhamini kwa fungu la
dhamana la 29.1 na hadi waendesha mashtaka wetu wanaondoka mahakamani
Dunga kufanikiwa kupata dhamana na kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 27,"
amesema Dunga.
Ametoa rai
kwa watanzania kuheshimu Katiba na Sheria ambazo wamejiwekea wenyewe na
pia wajifunze mafundisho mema katika misahafu inayofundisha kutii
mamlaka za Serikali zimewekwa na Mungu (BIBLIA, Warumi 13:1-2.)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...