Halmashauri
nchini zimetakiwa kuwatumia wataalamu wanaohitimu mafunzo ya mipango
miji na wapimaji wa ardhi mjini na vijijini ili kuweza kutatua migogoro
ya ardhi inayosababishwa na kutopimwa ardhi katika maeneo mbalimbali
kwenye Halmashari.
Wito
huo umetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel
Kalobelo wakati wa akimwakulisha Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,Nyumba na
maendeleo ya makazi Merry Makondo katika maafali ya 39 ya kutunuku vyeti
wahitimu wa fani mbalimbali wapatao 394 wa chuo cha Ardhi Morogoro.
Mhandisi
Kalobelo amesema kama wataalamu wanaozalishwa na vyuo Ardhi chini kama
watatumik vizuri na Halmashauri za Mikoa katika upimaji wa ardhi
migogoro mingi itapungua kwani kila mtu atakuwa anamiliki ardhi
iliyopimwa na kumilikiwa kisheria.
“Ni
aibu kwa Mkoa kama Morogoro kuendelea na migogoro ya ardhi wakati chuo
cha kuzalisha wataalamu wa kupanga na kupima kipo hapahapa. Naagiza
kabla ya mwaka huu kuisha Halmashauri zote za Mkoa wa Morogoro ziwe na
mpango mkakati wa kuona jinsi gani ya kushirikiana na chuo cha ardhi
Morogoro na kuhakikisha kila kipande cha ardhi kinapangwa,kupimwa na
kumilikishwa”.alisema Mhandisi Kalobelo.
Aidha
Mhandisi Kalobelo ametumia maafali hiyo kutoa wito kwa wadau,mamlaka na
tasisi mbalimbali kutenga fedha kwaajili ya kuweka mazingira wezeshi
kwa wataalamu wanaopima Ardhi kwenye Halmashauri zao.
Kwa
upande wake kaimu mkuu chuo cha Ardhi Huluma Lugala amesema chuo
kimeweza kuongeza udahili kutoka wananfunzi 400 mpaka kufikia wanafunzi
500 ikiwa ni ongezeko la asilimia 23 ya wananfunzi wote walioko chuoni
hapo.
Pia amesema mbali
na kuzalisha wataalamu wa kupanga na kupima pia chuo cha Ardhi Morogoro
kimekuwa kikishiriki katika kutoa huduma za ushauri wa kitaalamu na
kufanya miradi ya urasimishaji ambayo hadi sasa inatekelezwa katika
mikoa ya Dar es Salaam,Arusha na Morogoro.
Naye
Makamu mwenyekiti Bodi ya chuo Zakaria Ibrahim amesema kuwa chuo hicho
kimeendaa mpango mkakati wa mfumo wa mafunzo ambao utaweza kuzalisha
wataalamu wengi na wenye ujuzi zaidi katika masuala ya upimaji wa
Ardhi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...