Charles James, Michuzi TV

KATIBU Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Katanga ametoa siri ya namna alivyopokea uteuzi wake wa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi ambapo amemshukuru Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwa kumteua katika nafasi hiyo.

Balozi Katanga amesema leo ndio siku ambayo alitakiwa kurudi katika kituo chake cha kazi cha Ubalozi wa Tanzania nchini Japan lakini imembidi kuihairisha safari hiyo ili kuendelea na majukumu makubwa aliyokabidhiwa kwa sasa.

Amesema kazi kubwa ya kufanya ni kuhakikisha serikali iko makini katika kuendesha safari iliyoanza ya kufikia mwaka 2025 katika kuwaletea mafanikio na maendeleo nchi yetu.

" Jana nilishangaa nachukuliwa tu napelekwa huku na huko hadi uwanja wa ndege nikaambiwa nitulie hapa, natakiwa kwenda Dodoma hayo mengine ntayajua huko huko, basi nikiwa pale uwanja wa ndege ndio nikaona hotuba yako kwenye Televisheni ukiniteua, nashukuru sana.

Serikali yetu kupitia wizara zetu zina mahusiano, mfano Wizara ya Ujenzi ina mahusiano na Wizara ya Uchukuzi kwa sababu wizara ya ujenzi inavyomaliza kujenga uwanja wa ndege maana yake uchukuzi inatakiwa kuleta Ndege. Niahidi ushirikiano na uzalendo katika majukumu haya mapya," Amesema Balozi Katanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...