NA FARIDA SAID,MORGORO.
Wakazi
wa kata ya Mafisa Manispaa ya Morogoro wanalazimika kutembea umbali
mrefu kufuata huduma za afya nje ya kata hiyo kufuatia kituo cha afya
cha Sina ambacho kingetatua changamoto hiyo baada ya kushindwa
kukamilika kwa zaidi ya miaka 15 bila kumalizika kwa ujenzi wake mkoani
hapa.
Wakizungumza wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa
Umoja wa Wazazi wa CCM Morogoro Mjini katika kituo hicho mkoani hapa,
walisema kuwa kituo hicho kimekuwa kikisuasua kutokana na kutokamilika
kwa wakati jambo linalopelekea adha kwa wakazi wake kutembea umbali
mrefu kufuata huduma bora za kiafya.
Sabrina Rajabu
Mohamed alisema kuwa wakazi wa kata ya Mafisa wamekuwa wakipata adha
kubwa ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya ikiwemo za mama na
mtoto ambao hulazimika kutembea kufika katikati ya mji wa Manispaa ya
Morogoro kusaka vituo cha afya.
Ametaja vituo hivyo
ni pamoja na kituo cha Mwembesongo, Sabasaba, Nunge na Mfiga ambapo
wamekuwa wakipata huduma za mama na mtoto.
“Endapo
kituo cha afya Sina katika kata yetu hii ya Mafisa serikali
ingekabilisha kwa wakati adha ya sisi ya kutembea umbali mrefu
zingepungua lakini kwa sasa tunalazimika kutembea umbali mrefu kufuata
huduma za afya zaidi ya kilombeta tano hadi saba.”alisema Sabrina.
Diwani
wa kata ya Mafisa, Joel Kisome alisema kuwa kutokana na adha
wanayoipata wananchi wa kata hiyo ametoa kiasi cha sh45milioni kwa ajili
ya kumalizia ujenzi wa kituo hicho.“Nimetoa
sh45milioni kama sehemu ya mchango wangu wa kuchangia maendeleo katika
kata hii hasa katika kituo cha afya Sina lakini niiombe serikali
kuongeza nguvu ili kituo hiki kiweze kukamika na kutoa huduma.”alisema
Kisome.
Kisome alisema kuwa kukamilika kwa kituo
hicho kitapunguza adha ya wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma
za kiafya nje ya kata hiyo.
Alisema kuwa kukamilika
kwa kituo hicho kutasaidia wananchi wa kata ya Mafisa kupata huduma
karibu lakini na wananchi wa kata nyingine za jirani zikiwemo Tungi,
Kihonda na Lukobe.
Kwa upande wa Mwenyekiti huyo,
Salumu Kapira alisema kuwa amefurahishwa na kitendo cha diwani wa kata
hiyo kutoa fedha kumalizia baadhi ya mahitahi ya ujenzi huo.
Kapira
amewatoa shaka wakazi wa kata ya Mafisa kuwa serikali imejipanga
kumaliza kituo hicho cha Sina kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022 baada ya
halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kutenga sh50milioni.“Kazi
iliyopo kwetu kama viongozi ni kusimamia miradi ya maendeleo lakini
kuikumbusha serikali kwa ahadi ambazo zimetenga kwa ajili ya miradi
fedha zinafika kwa wakati.”alisema Kipira.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...