Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia
mara baada ya kuwaapisha MAkatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu na Wakuu
wa Taasisi Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne April 6, 2021
*Asema bango moja la mwananchi litaondoka na Mkurugenzi au Mkuu wa Wilaya
*Asisitiza umuhimu wa kukusanya kodi bila mabavu, ampa malekezo kamisha TRA
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa muelekezo
wa Serikali kwa kufafanua masuala mbalimbali huku akitwumia nafasi hiyo
kusisitiza watendaji na watumishi wa Umma kuhakikisha wanatimiza
majukumu yao.
Katika kusisitiza utendaji kazi Rais Samia ametumia
msemo wa kwamba anachotaka ni watu kufanya kazi na iwapo watazingua basi
watazinguana na kwamba anapotumia neno anaomba wajue kabisa ndio anatoa
maagizo na maelekezo.
Rais Samia amesema hayo leo Aprili 6 mwaka
2021 baada ya kuwaapisha Makatibu na Manaibu Makatibu Wakuu wa Wizara
mbalimbali.Aidha amewaapisha baadhi ya Makamishna na wakurugenzi wa
Taasisi na Mamalaka za Serikali.
Kuhusu suala la haki, Rais Samia
amesema kwamba nie vama watendaji na watumishi wa umma wakatenda haki
katika kuwatumia wananchi kwani ameshuhudia ziara za viongozi ambapo
kuna mabango mengi yanayozungumzia changamoto za watu.
"Haki za
wananchi, tunapokwenda kwenye ziara tunapokelewa na mabango na mabango
mengi yanayonekana yanayozungumzwa ni yale ambayo yanaweza
kushughulikiwa, bango moja aidha Mkurugenzi au Mkuu wa Wilaya
ataondoka.Nataka kusema hii isiwe sababu ya kuzuia wananchi wasioneshe
mabango yao.
"Tukipata malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa wamezuiwa
kuonesha mabango yao kwa viongozi tutachukua hatua.Shughulikieni
changamoto za wananchi kwenye maeneo yenu,"amesema Rais Samia wakati
akizungumzia utoaji haki kwa wananchi.
Kuhusu TAMISEMI, Rais
Samia ametumia nafasi hiyo kufafanua mambo mbalimbali katika kuhakikisha
TAMISEMI inaendelea kuwatumikia wananchi ambapo amewasisitiza kukusanya
kodi."Tunaomba mkakusanye kodi, TAMISEMI mkahakikishe mnakwenda
kukusanya kodi, Wizara kwa ujumla na TAMISEMI niwaombe muendelee kwenda
kusimamia ukusanyaji huo.
"Katika Ofisi ya Waziri Mkuu kulikuwa na
makatibu wakuu wawili au watatu, sasa nimeamua kupunguza na kuwa a
Katibu Mkuu mmoja na Manaibu wawili, mwanzo ilikuwa changamoto nani awe
ofisa masuhuli.Pia katika Ofisi ya Waziri Mkuu kuna ofisi binafsi ya
Waziri Mkuu fedha aliyokuwa anapelekewa ilikuwa inakatwa, hii si
heshima, naagiza fedha kwa ajili ya ofisi hiyo isikatwe,"amesema Rais
Samia.
Kuhusu vibali vya kazi ambavyo vinatolewa kwa waekezaji
wanaokuja nchini, amesema kumekuwa na changamoto kubwa katika utoaji wa
vibali vya kazi.Vibali vya kazi hapa kumekuwa na manyanyaso, ndipo eneo
ambalo watu wanatumia kuchuma fedha, anaomba kibali fedha zinamtoka.
"Vibali
vya kazi vimekuwa na changamoto, mtu anakuja na mradi binafsi anataka
kuweka mtu wake, mnasema hapana, tunaka mtu afurahie uwekezaji wa
Tanzania, kampuni zinafungwa na watu wanaondoka, kampuni zikifugwa na
fedha zinaondoka na ndio kilio cha watanzania mifukoni mitupu.Kama kuna
mtu anataka kuja kuwekeza na ana watu wake kwanini akatazwe na ndio
anayemuamini, acheni urasimu katika kutoa vibali, tunataka watu waje
kuwekeza,"amesisitiza.
Akifafanua zaidi amesema katika ofisi ya Waziri Mkuu kuna uwekezaji,hivyo ameagiza kuwepo na eneo moja ambalo kuna huduma zote, kwani nako kuna urasimu mkubwa."Hakuna wa kufanya maamuzi, kuna mzunguko mkubwa , hakuna mawasiliano kati ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaaa, naomba mnaosimamia uwekezaji nendeni mkae huko muondoke urasimu huu.
Akifafanua zaidi amesema katika ofisi ya Waziri Mkuu kuna uwekezaji,hivyo ameagiza kuwepo na eneo moja ambalo kuna huduma zote, kwani nako kuna urasimu mkubwa."Hakuna wa kufanya maamuzi, kuna mzunguko mkubwa , hakuna mawasiliano kati ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaaa, naomba mnaosimamia uwekezaji nendeni mkae huko muondoke urasimu huu.
"Lakini lingine ni kodi kwa wawekezaji, hakuna
uwiano kuhusu kodi, tumevishwa chapa kwamba Tanzania hatutabiriki,
naagiza mkanyooshe haya.Juzi tu nilitoa kauli kuhusu kodi, nimepokea
simu nyingi, naomba tuvute tena uwekezaji tupate kodi,"amesema.
Amesisitiza umuhimu wa kupunguza misuli kwenye eneo hilo la kodi."Sisi tunahitaji zaidi uwekezaji lazima tuangalie vizuri, tukafanye kazi, tukarudishe imani ya wawekezaji kuja kuwekeza Tanzania.Pia naomba mifumo ya fedha ikaangaliwe upya, lazima tujue mifumo yetu ya kukusanya fedha ni ipi."
Amesisitiza umuhimu wa kupunguza misuli kwenye eneo hilo la kodi."Sisi tunahitaji zaidi uwekezaji lazima tuangalie vizuri, tukafanye kazi, tukarudishe imani ya wawekezaji kuja kuwekeza Tanzania.Pia naomba mifumo ya fedha ikaangaliwe upya, lazima tujue mifumo yetu ya kukusanya fedha ni ipi."
Akizungumzia
miradi ya vipaumbele , amesema kuna urithi wa miradi ambayo wameachiwa
na Rais Hayati Dk.John Magufuli ambayo lazima itekelezwe na kukamilika
kama ilivyokusidiwa."Tuna mirathi ambayo tumeachiwa na aliyekuwa Rais
wetu, naomba sana sana twende tukasimamie miradi hiyo ya kimkakati.
"Kumuwepo na ucheleweshaji wa malipo tena kwa makusudi tu, kuna kipengele kinachozungumzia riba iwapo malipo yatachelewa, kinachoonekana wanaochelewesha malipo maana yake kuna mazungumzo hapo kati kati. Tunaongeza gharama za miradi, watu wa fedha nendeni mkasimmamie miradi iendelee vizuri."
Kuhusu Wizara ya Mambo ya Nje, Rais Samia amesema ameteua Waziri mwanamama Shupavu pamoja na Katibu Mkuu wake ambaye anaijua vizuri Wizara hiyo, hivyo ni matarajio yake watakwenda kukuza mahusiano kati yetu na mataifa ya nje."Wizara ya Mambo ya Nje mnafanya kazi kwa ajili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ni pande zote za muungano. Hakuna haja ya kuwekeana vigingi."
"Kumuwepo na ucheleweshaji wa malipo tena kwa makusudi tu, kuna kipengele kinachozungumzia riba iwapo malipo yatachelewa, kinachoonekana wanaochelewesha malipo maana yake kuna mazungumzo hapo kati kati. Tunaongeza gharama za miradi, watu wa fedha nendeni mkasimmamie miradi iendelee vizuri."
Kuhusu Wizara ya Mambo ya Nje, Rais Samia amesema ameteua Waziri mwanamama Shupavu pamoja na Katibu Mkuu wake ambaye anaijua vizuri Wizara hiyo, hivyo ni matarajio yake watakwenda kukuza mahusiano kati yetu na mataifa ya nje."Wizara ya Mambo ya Nje mnafanya kazi kwa ajili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ni pande zote za muungano. Hakuna haja ya kuwekeana vigingi."
Akizungumzia Tanzania ya
viwanda, Rais Samia amesema lazima Tanzania ya viwanda iwe inaeleweka
kwa watu, viwanda vingi vinakwenda mkoani na wilayani, hivyo lazima kuwe
na utaratibu wa kuwa na kanzu data ya kufuatilia maendeleo ya viwanda
hivyo vilipo na mwenendo wao.Aidha amezungumzia umuhimu wa kuendelea
kutafuta masoko yakiwemo ya mazao yanayozalishwa nchini.
Kwa upande
wa madini ,Rais Samia amesema kuna haja ya kufanyika kwa majadiliano
katika kuhakikisha madini yaliyopo nchini yaachimbwa na kuwanufaisha
Watanzania wote."Kwenye madini najua tuna ubia na kampuni za nje, najua
Barick tunashirikiana nao kupitia kampuni ya Twiga.Katika eneo hili la
madini kama kuna kodi za kusamehe tusamehe.
"Kwenye mazungumzo
yafanyike mapema kupita Kamati za majadiliano ili tuanze kufanya kazi
na nchi ifaidike.Uchimbaji maeneo ya hifadhi, najua kuna madini katika
maeneo ya TANAPA , madini yachimbwe maana hata yakikaa kwenye hifadhi
tembo hawali madini.
"Mirerani tumejenga ukuta , tumeweka na majeshi
lakini madini yanatoka kama mwanzo, tukabaini madini ndio utanaota
yanapigwa picha na Rais, tuweke udhibiti katika madini, yanaendelea
kuibwa.
"Lakini kwenye kitalu C sitaki kuona mkono wa mtu, wapo
walianza kugawa kile kitalu waache, kuna matumizi yake,"amesema na
kuongeza "Madini yetu ndio tegemeo letu kwenye nchi, tusiposimamia
vizuri tunashusha uchumi wetu, simamieni vizuri.
Kwa upande wa Wizara
ya Ardhi, Rais Samia amesema bado kuna dhuluma kubwa ambayo inafanyika
katika kudhulum ardhi za watu na baadhi wanaofanya dhuluma hiyo na
maofisa ardhi, hivyo ameagiza eneo hilo liangaliwe kwa umakini.
Wakati
katika Wizara ya Maji, amesema iwe mvua, iwe jua lazima maji yapatikane
asilimia 95 kwa mijini na asilimia 85 kwa maeneo ya vijijini."Mtakwenda
kufanya nini mtajua wenyewe, lakini ikifika mwaka 2025 maji lazima
yapatikane kwa kiwango kinachotakiwa, tunadeni kubwa kwa wananchi kwenye
maji"
Katika Wizara ya Habari, Sanaa ,Utamaduni na Michezo , ametoa
maagizo kuhakikisha vyombo vya habari ambavyo vimefungiwa na hasa
televisheni za mtandaoni, zifunguliwe lakini sheria na kanuni zifuatwe
na adhabu ambazo zitatolewa ziwe wazi ili kila mmoja ajue.
Aidha
amesema kuna haja ya kuwekwa kwa mazingira mazuri kwa wasanii na
wanamichezo kwani ni eneo ambalo linaajiri wananchi wengi.Pamoja na hayo
amesisitiza umuhimu wa maeneo yote ya utumishi wa umma kutimiza
majukumu yake huku akitumia msemo kwamba yeye ni Mama lakini
atakayezingua basi watazinguana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...