Na Amiri Kilagalila,Njombe
Timu
ya watu 55 ikiongozwa na mkuu wa mkoa wa Songwe brigedia Nicodemas
Mwangela imehitimisha ziara ya siku tatu wilayani Njombe ya mafunzo kwa
vitendo ya utekelezaji wa kampeni ya usafi wa mazingira na ujenzi wa
vyoo bora na vya kisasa ambayo haifanyi vyema katika mkoa huo
ulionzishwa mwaka 2016.
Shabaha
ya ujio wa timu hiyo mkoani Njombe ni kujifunza mbinu zilizotumiwa na
timu nzima ya utekelezaji wa kampeni hiyo pamoja na wananchi na kuifanya
halmashauri ya wilaya ya Njombe kuendelea kuwa kinara katika mashindano
ya kitaifa mfururizo katika utekelezaji wa kampeni ya maji na usafi wa
mazingira.
Wakizungumza
mara baada ya kutembelea vijiji tofauti vya halmashauri ya wilaya ya
Njombe na kisha kuelezwa njia walizotumia kufikia mafanikio katika
utekelezaji,viongozi na watalaamu wa idara ya afya mkoa wa Songwe
akiwemo Samwel Opulukwa ambaye ni mkuu wa wilaya ya Songwe,Dkt Seif
Shakalage na Dkt Hamad Nyembea ambaye ni mganga mkuu wa mkoa wa Songwe
wanasema ni kupunguza mabavu na badala yake elimu na makubaliano ndiyo
yamefanya wakazi wa Njombe kujenga vyoo bora kwa hiari.
Kwa
niaba ya mkuu wa mkoa wa Songwe,katibu tawala wa mkoa huo Dkt, Seif
Shakalage amewahakikishia UNICEF pamoja na mkoa wa Njombe utayari wao wa
kwenda kutekezeza zoezi hilo kikamilifu ili kuufikia mkoa wa Njombe.
“Katika
mkoa wa Songwe watu kuwa na vyoo tuna asilimia 99.6% kwa hiyo
tunapokuja kujifunza hapa ni kwajili ya kumalizia kazi yetu,mimi ninayo
timu nzuri kwa hiyo tunaenda kumalizia kazi iliyobaki”alisema Shekalage
Aidha
amewashukuru viongozi wa mkoa wa Njombe kwa ushirikiano waliouonyesha
katika kuwajengea uwezo wa zoezi hilo lililoleta mafanikio wilaya ya
Njombe.
Naye katibu
tawala wa mkoa wa Njombe Katarina Revocat kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa
Njombe,amewaomba shirika la UNICEF wafadhili wa mradi wa utekelezaji wa
zoezi la usafi wa mazingira kuongeza wigo wa maeneo ya utekelezaji wa
mradi zaidi ya wilaya mbili kama ilivyo sasa ukilinganisha na mkoa wa
Songwe unakotekelezwa mkoa wote.
“Tunawaomba
UNICEF mtengeneze uwanja sawa,mkoa wa Songwe unakwenda kama mkoa mzima
lakini Njombe mnasapoti wilaya mbili hapa mtusaidie kidogo”alisema
Revocat
Aidha amepongeza
mkoa wa Songwe kwa ujasili wa kujitoa na kuja kujifunza katika mkoa wa
Njombe huku akiwashukuru wataalamu wa mkoa wa Njomnbe walioshiriki na
kusadia kutoa elimu kwa wageni hao.
“Nawashukuru
sana ndugu zangu wa Njombe kuweza kupokea wageni,mpaka sasa hivi
wanaondoka wakiwa wanakumbuka ile huduma mliyoitoa hongereni
sana”alisema Revocat
Frenk
Odhiambo ni mkuu wa kitengo cha maji na usafi wa Mazingira kutoka
UNICEF amesema anatarajia mafanikio makubwa kutoka mkoa wa Songwe
kutokana na ushirikianao wao huku akiadi kwa niaba ya shirika kuwa bega
kwa bega na serikali ya Tanzania katika kuendeleza shughuli zinazofanywa
na shirika ili kuisadia jamii ya watanzania.
Idadi
kubwa ya vyoo vya kaya za mkoa wa Songwe Vipo daraja A na B ambayo si
bora kiafya huku Njombe hususani katika halmashauri ya wilaya ya Njombe
vikiwa katika ngazi ya juu na salama kiafya ambayo C na D.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...