Na Pamela Mollel,Arusha
Oparesheni maalum ya kusaka vifungashio na mifuko iliyo chini ya kiwango imebaini ujanja unaotumika na wazalishaji kwa kuchanganya katikati vifungashio vyenye ubora na visivyo na ubora kwa kuhofia kukamatwa
Akizungumza leo jijini Arusha,Mkaguzi wa mazingira kutoka Baraza la Taifa la hifadhi ya mazingira Kanda ya kaskazini Justine Kasoka alisema kuwa katika oparesheni hiyo wamebaini udanganyifu unaofanywa na wazalishaji wa vifungashio hivyo kwa kuchanganya na visivyokuwa na ubora
Aliongeza kuwa wazalishaji wanachanganya vifungashio vyenye nembo na taarifa zinazotoa maelezo na vile ambavyo havina kabisa yaarifa yoyote sehemu vinapotoka jambo ambalo ni kinyume na sheri
Aidha alitoa Rai kwa makampuni na viwanda vinavyozalisha mifuko mbadala kuhakikisha wanazingatia sheria inavyowaelekeza kwa kuweka chapa pamoja na maelekezo yote yanazingatiwa kwa kuwa zoezi la ukamataji limeanza rasmi na yule asiyezingatia maelekezo hatua Kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake
Alisema mifuko yote mbadala isiyokuwa na nembo na taarifa kamili inapotoka pamoja na nembo ya Shirika la Viwango Nchini ( TBS) ikiwa ni pamoja na mifuko laini isiyokidhi viwango hairuhusiwi na tayari zoezi la ukamataji limeanza kwa wafanyabiashara wanaokiuka taratibu na sheria ya mazingira.
Aliwapongeza wananchi wa jiji la Arusha kwa kutokomeza mifuko hiyo kwa kiwango kikubwa huku akisema katika zoezi hilo wamebaini kuwa wafanyabiashara wadogo wadogo waliowengi hawakukutwa na vifungashio vilivyochini ya kiwango isipokuwa wachache walionunua bila kugundua kuwa ndani vimechanganyikana na visivyohitajika .
Naye mfanya biashara wa viungo soko la kilombero Celina Fredy aliiomba Serikali iwakumbuke walaji wachini ili kuwepo na vifungashio vya bei ya chini vinavyoendana na hali yao.
Zoezi hilo lilifanyika katika eneo la Soko kuu,Soko la Kilombero na Soko la Samunge
Kushoto ni Mkaguzi wa mazingira kutoka Baraza la Taifa la hifadhi ya mazingira Kanda ya kaskazini Justine Kasoka akifanya ukaguzi wa mifuko iliyochini ya ubora katika oparesheni maalumu iliyofanyika katika soko la Kilombero jijini Arusha,katikati ni Afisa Nemc Alpha Laizer wakishirikiana katika ukaguzi huo
Katikati ni Afisa Mazingira Mkuu wa Baraza la Taifa la hifadhi ya mazingira,Salim Salum akitoa elimu kwa mfanyabiashara Mara baada ya kukutwa akitumia mifuko iliyochini ya ubora,kushoto ni Mkaguzi wa NEMC kanda ya kaskazini Jastine Kasoka
Mkaguzi wa mazingira kutoka Baraza la Taifa la hifadhi ya mazingira Kanda ya kaskazini Justine Kasoka katikati akizungumza na vyombo vya habari kuhusu oparesheni kabambe ya kutokomeza mifuko na vifungashio vilivyo chini ya viwango na kuwa wamebaini udanganyifu unaofanywa na wazalishaji wa vifungashio hivyo kwa kuchanganya na visivyokuwa na ubora
Mfanyabiasha wa mifuko na vifungashio akionyeshe mifuko yake kwa maafisa wa Baraza laTaifa la hifadhi ya Mazingira waliofika kukagua mifuko iliyochini ya kiwango
Afisa kutoka Nemc Alpha Laizer akionyesha mfuko unaofaa kwa matumizi
Maafisa wa Baraza la Taifa la hifadhi ya Mazingira wakiwa katika picha ya pamoja
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...