Na Mwaandishi Wetu Mtwara

MKUU wa Wilaya ya Mtwara Danstan Kyobya ameeleza kusikitishwa na taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa hali kimbunga Jobo kimeshafika Mtwara na kufanya madhara.

Akiongea na waandishi wa habari ofisin kwake jana kuhusu hali ya hewa ya Mkoa wa Mtwara, Kyobya amesema wanaosambaza taarifa hizo wana nia mbaya na nchi na kwa Mtwara na kuwaomba wananchi wa mkoa wa Mtwara na Watanzania kuzipuuuza taarifa hizo kwan hali ya hewa kwa Mtwara ni nzuri na kwamba hakuna madhara yoyote ambayo yametokea kutokana na Kimbunga Jobo.

“Mtwara ni salama, hakuna upepo, kuna mvua za hapa na pale ambazo hazina madhara yoyote. Nisikitike kwamba kuna watu ambao wana nia zmbaya na Mtwara, Wana nia mbaya nan chi yetu ya Tanzania wanasambaza clip kuonyesha kwamba mtwara kuna jobo imeshafik kwa maana ya kimbunga cha jobo kimeshafika kitu ambacho sio kweli kabisa,” amesema.

Amesema Wilaya zote za Mtwara hali ya hewa ni nzuri, na kwamba Mtwara kuko salama na kwamba kuna hali ya mvua ya kaweida ambayo haina madhara wala upepo ambao unatishia hali ya amani.

Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA) Kanda ya Kusini imekanusha uwepo wa hali ya hewa mbaya katika mikoa ya Lindi na Mtwara kufuatia taarifa za uwepo wa Kimbunga Jobo kilicho bahari ya Hindi.

Meneja wa Kanda hiyo Amas Daudi amewaambia waandishi wa habari mkoani hapa kuwa ofisi yake inaendelea kufuatilia na kwamba hakuna hali ya hewa mbaya ambayo imeshuhudiwa mpaka sasa.

“Mpka sasa  hivi hatujashuhudia hali ya hewa mbaya hapa Mtwara na ukiangalia picha za satellite, ni kwamba  kuna mawingu yako baharini yanajaribu kusongea kuja kwetu huku baadae kunaweza kukawa na ongezeko la mvua tu,” amesema.

Meneja huyo amesema kuwa amepiga simu Kilwa Masoko  na kutaarifiwa kuwa kuna mvua mvua za kaweida. Kwa upande wa Lindi Mjini, Daudi amesema kuwa pia hali ni ya kaweida na kwamba kuna manyumanyu yanaendelea.

Katika hatua nyingine, wavuvi wa manispaa ya Mtwara wameipongeza TMA kwa kutoa taarifa mara kwa mara kuhusu uelekeo wa kimbunga Jobo kilicho bahari ya Hindi.

“Kwanza nawapongeza sana TMA kwa kuona umuhimu wa kutoa taarifa mara kwa mara kuhusu kimbunga Jobo huku baharini, hii inatusaidia sana sisi kujua nini tufanye na kwa wakati gani, mfano kwenye taarifa ya TMA, kila wakitoa taarifa yao wanasema upepo wa kimbuga kilomita ngapi, hii inatusaidia sana,” amesema Mwenyekiti wa Wavuvi Manispaa ya Mtwara Shekhe Shamte.

Amesema wavuvi bado wanaendelea na shughuli zao za kuvua samaki na kwamba hawajaacha isipokuwa wanachukua tahadhari kwa kuacha kwenda mbali wakati wakivua samaki.


Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Danstan Kyobya (Katikati) akiongea na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu taarifa zinazosambaa mitandaoni zikionyesha kuwa Kimbunga Jobo kilichopo Bahari ya Hindi kimefika Mtwara na kusababisha madhara.
Baadhi ya Wavuvi wa Manispaa ya Mtwara wakiandaa nyavu zao Kwa ajili ya kwenda kuvua samaki hapo kesho mapema. Wavuvi hao wamepunguza safari za baharini ili kuchukua tahadhar kutokana na uwepo wa Kimbunga Jobo Bahari ya Hindi

Shughuli zikiendelea katika pwani ya Manispaa ya Mtwara Soko La Feri
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...