Charles James, Michuzi TV

WAMEAMINIWA! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mawaziri watano wanawake kuaminiwa katika Baraza la Mawaziri na Rais Mama Samia Suluhu Hassan.

Rais Mama Samia jana alifanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri ambapo wapo mawaziri wameendelea kuhudumu katika nafasi zao zilezile walizokua nazo kwenye uongozi wa aliyekua Rais Hayati Dk John Magufuli huku wengine wakihamishwa na wengine wakiteuliwa.

Katika mabadiliko hayo madogo yaliyofanyika mawaziri kamili wanawake ni watano tofauti na Baraza lililopita kabla ya mabadiliko hayo ambapo mawaziri kamili wanawake walikua ni wanne.

Mawaziri Wanawake walioingia kwenye Baraza hili la Rais Mama Samia ni pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama ambaye ameendelea kuwepo hapo hapo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Ummy Mwalimu ambaye awali alikua Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano na Dk Dorothy Gwajima ambaye ameendelea kuwa Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto.

Wengine ni Prof Joyce Ndalichako ambaye ameendelea kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Balozi Liberrata Mulamula  ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akichukua nafasi ya Prof Palamagamba Kabudi aliyehamishiwa Wizara ya Katiba na Sheria.

Rais Mama Samia amewataka wote walioteuliwa kushika wadhfa huo kufanya kazi kwa bidii na yeyote ambaye atashindwa kutekeleza majukumu yake kikatiba hatosita kutengua uteuzi wake.

Balozi Mulamula ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa na Rais Mstaafu wa Marekani Mhe.Baraka Obama.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...