Wanafunzi wanufaika wa mpango wa ufadhili wa masomo ya kilimo unaotolewa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) maarufu kama Kilimo Viwanda kutoka katika chuo cha Mt. Maria Goretti wamepata fursa ya kuembelea shamba la Silverlands lililopo Ifunda mkoani Iringa.

Wanafunzi hao ambao waliambatana na waalimu wao waliungana na baadhi ya wafanyakazi wa SBL akiwamo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Mark Ocitti, Mkurugenzi wa Mahusiano kwa Umma John Wanyancha na wafanyakazi wengine.

Mkurugenzi huyo alisema kampuni ya SBL imedhamiria kuendelea kutengeneza maisha bora kwa vijana na wakulima nchini kupitia programu yake ya udhamini wa masomo kwa wanafunzi wanaotoka familia masikini kwenye vyuo vinavyofundisha kilimo.

Programu hii iliyoanzishwa mwaka 2010 imesaidia wanafunzi 71 kusomea kozi za diploma katika ujuzi wa kilimo katika vyuo vinne kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa SBL, Mark Ocitti.

Mkurugenzi huyo kuwa Kilimo Viwanda imelenga kusaidia wanafunzi kutoka familia masikini ili waweze kusomea masomo ya kilimo kwenye ngazi ya diploma katika vyuo vya ndani.

Wanafunzi wengine 43 chini ya programu hii wanapatikana Kaole Wazazi College of Agriculture (Bagamoyo), Kilacha Agriculture and Livestock Training Institute (Moshi) na Igabiro Training Insitute of Agriculture (Bukoba).

Ocitti alifafanua kuwa ufadhili huu unajumuisha malipo yote ya chuo na gharama zingine katika kipindi chao chote cha masomo. Vilevile, Kilimo Viwanda inalenga kuongeza nguvu jitihada za Serikali katika kuimarisha sekta ya kilimo kwa kuongeza idadi ya wataalamu wa mashamba watakaowasaidia wakulima kuboresha mashamba yao. SBL inategemea kwa kiasi kikubwa mazao ya nafaka kama vile mtama, shayiri na mahindi katika uzalishaji wao.

Vilevile Ocitti alisema, ‘Programu hii ni fursa nzuri kwa wanafunzi kuongeza upeo wao kwa kujifunza kimatendo watakapotembelea mashamba makubwa ya wakulima wanaolima nafaka kama hizi pamoja na kutembelea viwanda vyetu vya Dar es Salaam, Moshi na Mwanza ili kushuhudia namna kilimo na uzalishaji unavyotegemeana.’

Meneja wa shamba la Siverlands lililopo Ifunda mkoani Iringa WayneTraves (aliyechuchumaa) akiwaelekeza jambo kuhusu udongo wanafunzi wa Chuo cha Kilimo cha Mt. Maria Goretti Pamoja na wafanyakazi wa SBLikiwamo Mkurugenzi Mtendaji Mark Ocitti (aliyevaa kofia) walipotembelea shamba hilo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti  (SBL) Mark Ocitti (aliyevaa kofia) akiongea na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kumalizika kwa ziara ya wanafunzi wa Chuo cha Kilimo cha Mt. Maria Goretti ambao ni wanufaika wa Programu ya ufadhili wa masomo wa kampuni hiyo unaojulikana kama Kilimo Viwanda katika shamba la Silverlands lililopo Ifunda mkoani Iringa. Kulia aliyevaa miwani ni mmoja wa wafanyakazi wa shamba hilo Janet Senders

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti  (SBL) Mark Ocitti (aliyevaa kofia) akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo cha Kilimo cha Mt. Maria Goretti ambao ni wanufaika wa Programu ya ufadhili wa masomo wa kampuni hiyo unaojulikana kama Kilimo Viwanda katika muda mfupi baada ya kumalizika kwa ziara katika shamba la Silverlands lililopo Ifunda mkoani Iringa. Wengine kwenye picha ni wafanyakazi wa shamba hilo na wafanyakazi wa SBL

 



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...