Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
MADIWANI
wa halmashauri ya Bagamoyo ,wamedhamiria kulifufua Shirika la maendeleo
ya Bagamoyo (BADECO ) ,kuwa sehemu ya mradi mkakati kusaidia kuinua
uchumi na kuongeza pato la ndani la halmashauri hiyo .
Eneo
hili lilikuwa kitambulisho cha wilaya kwakuwa kivutio ikiwemo watalii
lakini kutokana changamoto mbalimbali lilikufa na sasa imebakia magofu
na baadhi ya watu wakiendelea kujinufaisha kiholela bila
utaratibu,";Anasema mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Muhammed
Usinga.
Usinga ambae pia
ni diwani wa kata ya Yombo akielezea kuhusu walivyojipanga kuibua vyanzo
vipya na kufufua maeneo ya kiuchumi ili kujiongezea mapato ,alisema
Badeco inapaswa kufufuliwa kwa manufaa ya wilaya.
Alieleza
kuwa ,hatua wanayoichukua kwanza ni kutoa matangazo kukaribisha wadau
na wawekezaji watakaokaa nao meza moja kuona namna ya kutimiza lengo lao
.
"Tunatarajia kuongeza
vyanzo vya mapato ya halmashauri na maeneo ya utalii ,":;hivyo basi
Usinga amewaomba wawekezaji wajitokeze kuijenga BADECO mpya kwa kufuata
maelekezo ya wataalamu wa halmashauri.
Nae
diwani wa kata ya Dunda ,Hafsa Kilingo alisema, BADECO maarufu kama
BADECO Beach ilikuwa gumzo nchini ambayo watu wengi walikuwa wakitoka
maeneo mbalimbali kwenda kwenye kivutio hicho .
Hafsa
alitaka wawe na msimamo wa kweli ,na kuacha kuangalia walipotoka na
badala yake wasimamie mipango waliyojiwekea ili kuinua pato la
halmashauri na maendeleo ya wilaya.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainab Kawawa alisisitiza kuibuliwa kwa vyanzo vipya vya mapato.Alibainisha kwamba , moja ya vyanzo vinavyopigiwa kelele bila matokeo ni BADECO .
Zainab
alisema ,ameshazungumzia sana kuhusu suala hilo ambapo watendaji na
madiwani wa halmashauri wanatakiwa kulisimamia na kuchukua hatua kwa
maslahi ya wilaya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...