Mwenyekiti wa Bawacha, Suzan Kiwanga akizungumza na waandishi wa habari Mkoa wa Dar es Salaam leo.
Wanawake Chadema wakiwa na Mabango
Baadhi ya wanawake wa Bawacha Chadema katika mkutano na waandishi wa habari Mkoani Dar es Salaam leo.
Wanawake chadema wakiimba katika Mkutano na waandishi wa habari leo.

BARAZA la Wanawake Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) lawakana wabunge wanawake wa 19 waliopo katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani wamekosa sifa ya kuwa wabunge kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 67 (1) (b).

Akizungumza na waandishi wa habari Mkoa wa Dar es Salaam leo Mei 4, 2021 Mwenyekiti wa Bawacha, Suzan Kiwanga amesema kuwa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekiukwa kwani imeweka masharti na sifa za mtu kuteuliewa kuwa Mbunge kwani ni lazima awe amependekezwa na Chama cha siasa.

"Sisi ajenda yetu tunayo wabunge 19 sio halali anaowaita wabunge wale ni vibaka tuu, wabinafsi, wasaliti, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lazima waondoke bungeni."Amesema Suzan

Suzan amesema kuwa suala la wabunge 19 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni suala la kikatiba sio suala la utashi wa Spika wa bunge, hata hivyo wamemwomba spika wa Bunge aelekeze matakwa ya kikatiba mara moja, na masharti kikatiba na sio kuwatetea ingali inajulikana.

Kwa Mujibu wa Maneno ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai alisema Jana Mei 3,2021 "Je hawa wabunge 19 wanaotuhumiwa kufuzwa je walipata hata nafasi ya kuhojiwa? je walipata nafasi ya kujieleza? je, walipata Natural Justice? Walisikilizwa? nifukuze watu ambao hawajasikilizwa popote?.

Hata hivyo Bawacha wamesema walimuandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwaajili ya kupewa nafasi ya kusikilizwa na kuzungumza suala la maridhiano kati ya wanachama wa Chadema na wabunge 19 waliopo bungeni bila kuwa na Chama.

"Suala la Maridhiano ni baina ya Chadema na Rais ni kutambua Umhimu wake, na Rais akakubali hivyo halina Uhusiano wowote na Spika wa Bunge. Baraza la wanawake Chadema tunaona kama Spika ana lengo la kuvuruga mazungumzo hayo huenda akawa na manufaa binafsi kuona nchi iliyogawanyika." Amesema Suzan

Amesema kuwa utaratibu wa upatikanaji wa wabunge vitu maalumu kwenye Chama cha Demokrasia na Maendeleo huanzia ngazi ya chini kabisa kabla ya kufikia kamati ya utendaji na kisha sekretarieti ya baraza la wanawake Chadema na baadae hupelekwa kwenye kamati kuu ambayo hupitisha majina hayo na kuwasilisha katika tume ya Taifa ya Uchaguzi.

"Hivyo basi wanaoitwa wabunge 19 kujichagua na kujipeleka kwenda kuapa sio tu kwamba ni uvunjaji wa katiba ya chama bali ni ubinafsi, usaliti na uasi wa kiwango cha juu." Amesema Susan

Licha ya hayo Suzan amezitaka kamati tendaji BAWACHA kukutana kwaajili kujadiliana na hatua sitahiki za kuchukua juu ya suala la wabunge 19 waliopo bungeni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...