Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Fedha na Uchumi pamoja na Mkutano wa Mawaziri wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Mashauriano ya Kibajeti unafanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 3 hadi 7 Mei 2021.
Mkutano huo ambao umeitishwa na Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, umetanguliwa
na kikao cha Ngazi ya Wataalam kutoka Sekta za Fedha na Uchumi unaofanyika
kuanzia tarehe 3 hadi 5 Mei 2021 na kufuatiwa na kikao cha Makatibu Wakuu tarehe 6 Mei 2021 kabla ya kuhitimishwa na Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri
mnamo tarehe 7 Mei 2021.
Mkutano huo wa 12 pamoja na mambo mengine una lengo la kupokea na kujadili taarifa za Kamati
zinazoshughulikia masuala ya Fedha pamoja na kufanya mashauriano ya awali ya Bajeti
ya Mawaziri wa Fedha na masuala ya Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Vilevile, utapokea Taarifa ya Utekelezaji wa Maazimio mbalimbali
yaliyofikiwa wakati wa Mkutano wa 11 wa Baraza hilo la Kisekta.
Ujumbe wa Tanzania kwenye kikao cha ngazi ya Wataalam unaongozwa na Bw. William Mhoja,
Kamishna wa Uchambuzi wa Sera kutoka Wizara ya Fedha na Mipango.
Bw. James Msina, Kamishna Msaidizi, Idara ya Fedha za Nje anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Kikanda kutoka Wizara ya Fedha na Mipango akichangia jambo wakati wa kikao cha wataalam wanaoandaa Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Sehemu
ya Wajumbe wa kikao cha Wataalam wakiwa wamesimama kabla ya kuanza
kikao chao ili kumkumbuka aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliyefariki dunia mwezi
Machi 2021
Kamishna
wa Uchambuzi wa Sera kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. William
Mhoja (kushoto) akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano wa
majadiliano kwa ngazi ya wataalam ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa 12
wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Fedha na
Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika jijini Arusha tarehe
7 Mei 2021. Mkutano wa Wataalam unafanyika kuanzia tarehe 3 hadi 5 Mei
2021 na kufuatiwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu tarehe 6 Mei 2021. Kulia
ni Bw. James Msina, Kamishna Msaidizi, Idara ya Fedha za Nje
anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Kikanda, Wizara ya Fedha na
Mipango.
Mkuu wa Idara inayoshughulikia masuala ya Fedha katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Pantaleo Kessy (kushoto) akichangia jambo wakati wa kikao cha wataalam
Ujumbe kutoka Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Uganda wakishiriki mkutano wa ngazi ya wataalam ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika jijini Arusha tarehe 7 Mei 2021
Mjumbe kutoka Burundi akishiriki mkutano wa wataalam
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Elias Bagumhe akishauriana jambo na mjumbe kutoka Tanzania wakati wa kikao cha wataalam
Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia majadiliano yaliyokuwa yakiendelea
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania kwenye kikao hicho
Ujumbe ulioshiriki kikao cha waatalam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...