Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akimpa pole na kumfariji Bibi Leah Mahibwa (50) Mkazi wa Manyoni aliyelazwa kwa Matibabu katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma, wakati Makamu wa Rais alipofika katika Hospitali hiyo leo Mei 04,2021. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor
Mpango, akisalimiana na kuwapa pole Wananchi mbalimbali waliofika katika
Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma kwa ajili ya kupatiwa
Matibabu wakati Makamu wa Rais alipofika katika Hospitali hiyo leo Mei
04,2021.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor
Mpango, akipata maelezo kutoka kwa Daktari wa mambo ya Neuron Surgery
Dr. Humba, kuhusu maendeleo ya Matibabu ya Bibi Zaveria Chuga Malamba
(62) Mkazi wa Dodoma aliyelazwa kwa Matibabu katika Hospitali ya
Benjamin Mkapa Jijini Dodoma, wakati Makamu wa Rais alipofika katika
Hospitali hiyo leo Mei 04,2021.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akisindikizwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango, alipokuwa akiondoka katika Uwanja wa Ndege
Jijini Dodoma leo Mei 04,2021 kuelekea Nchini Kenya kwea Ziara ya Siku
mbili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...