Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Dkt Leonard Chamuriho   amesema ujenzi wa  Meli ya Mv Mwanza Hapakazi tu ambao hadi sasa umefikia asilimia 74 utakamilika baadaye mwakani.

 Waziri Chamuriho ameyasema hayo leo jijini Mwanza alipokuwa akikagua ujenzi wa meli hiyo ya kisasa  inayojengwa na Kampuni ya Gas Ente kutoka Korea ya kusini ikishirikiana na Kaang Nam Corperation pamoja na Suma JKT.

 Aidha Waziri Chamuriho amesema ujenzi wa meli hiyo ni moja  ya miradi mikubwa minne inayotekelezwa na   kampuni ya huduma za Meli  Nchini (MSCL) na kusimamiwa na  Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi. 

 “Miradi  mengine inayotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa  ni pamoja na ukarabati  wa Meli ya New Victoria,Ujenzi wa MV Butiama pamoja na Chelezo  ambayo ujenzi wake umekamilika”, amesema Chamuriho.

 Katika hatua nyingine Waziri Chamuriho amesema Wizara pia imejipanga kuendeleza miradi mingine katika Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa ikiwemo mradi wa Ukarabati wa meli kongwe ya MV Liyemba .

 Kwa upande wake Msimamizi wa mradi wa ujenzi wa Mv Mwanza  Mhandisi Vitus Mapunda amesema  Ujenzi huo umeajiri Zaidi ya watumishi 180 katika kada mbalimbali  na utakapokamilika utaleta fursa nyingi za ajira nchini.

 Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa Huduma za Meli (MSCL) Philemon  Bagambilana amesema  kampuni imejipanga kuboresha  na kutoa huduma  bora katika  usafiri  wa majini kwenye Ziwa Victoria, Ziwa Nyasa, Ziwa Tanganyika na kupanua huduma kwenye  Bahari ya Hindi.

Muonekano wa Meli ya Mv -Mwanza Hapa Kazi tu inavyoendelea kujengwa  na  hadi sasa ujenzi  wake umefikia asilimia 74 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwaka 2022.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Dkt Leonard Chamuriho akipanda ngazi kwenda  kukagua ujenzi wa Meli Mpya ya Mv  Mwanza Hapa kazi tu ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 74 na  inatarajia kukamilika mwaka 2022 na itakapokamilika itakuwa na uwezo wa kuchukua abiria 1200 na mizigo tani 400.

Waziri  wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Dkt.Leonard Chamuriho (wa katikati) akitoa maelekezo kwa wahandisi wanawake wanaoshiriki katika ujezi wa Meli Mpya  ya Mv- Mwanza Hapa Kazi Tu.

Mafundi wa kampuni ya Ges Entec ya Korea ya Kusini wakiendelea na kazi ya kuchomelea sehemu ya Nje ya Meli ya Mv  Mwanza Hapa Kazi Tu, Ujenzi wa Meli hiyo unatarajiwa kukamilika Mwakani.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Huduma za Meli Nchini (MSCL) Bw, Philemon Bagambilana akitoa maelezo  kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt Leonard Chamuriho  mara baada ya kukagua ujenzi wa Meli mpya ya Mv Mwanza hapa kazi tu.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...