Meneja wa Wateja Maalum wa Tigo, Mary Rutta akimkabidhi mfano wa Hundi ya Kiasi cha Milioni 1 Johari Ally Shabani miongoni mwa washindi 10 akisherehekea zamu yake kushinda pesa na Tigo.



WASHINDI wa wiki ya sita ya Promosheni Sherehekea Pesa, inayoendeshwa na Kampuni ya Mawasiliano - Tigo, jana wamekabidhidwa zawadi zao. Hadi sasa, Tigo imeshakabidhi, zawadi za jumla ya sh. milioni 60 kwa washindi 60 wa kila wiki. Katika promosheni ya Sherehekea Pesa inayoendelea, washindi 10 hupatikana kila wiki, ambapo kiasi cha zaidi ya sh. milioni 200 zitatolewa kwa washindi wote watakaoibuka kidedea. Promosheni ya Sherehekea Pesa ni sehemu ya sherehe ya miaka 10 ya kampeni ya Tigo Pesa nchini Tanzania. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana wakati wa hafla ya kukabidhi fedha, Meneja wa Wateja Maalum wa Tigo, Mary Rutta, alisema ni wiki ya sita sasa wateja wa Tigo Pesa kutoka sehemu mbalimbali, wamezidi kujishindia pesa taslimu katika Promosheni ya Sherehekea Pesa. "Droo hii inafanyika kila wiki na washindi wanajipatia fedha taslimu. “Vile mteja wa Tigo anavyotumia Tigo Pesa kwa kulipa malipo ya bili, manunuzi ya bidhaa na huduma, kutuma pesa kwa wateja wengine wa Tigo Pesa, kupokea pesa kutoka benki, mitandao mingine na nchi zingine, ndivyo wanavyopata nafasi zaidi kushinda zawadi za pesa. ” alisema Mary. Alisema washindi wa fedha ya kila wiki, wanatoka katika mikoa mbalimbali wanaingia kwenye promosheni hiyo ya kila wiki ambapo promosheni itaendelea kwa wiki nne zaidi kutoka sasa na kila wiki washindi 10 watakabidhiwa zawadi zao 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...