ALIYEKUWA Katibu wa chama cha Walimu Tanzania (CWT) Deus Seif na Mwekahazina wake, Abubakar Allawi, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka mawili likiwemo la matumizi mabaya ya madaraka na kujipatia zaidi ya Sh milioni 13.9.
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Imani Nitume mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Rashid Chaungu imedai washtakiwa walitenda makosa hayo kati ya Oktoba 3 hadi Novemba 6 mwaka 2018 jijini Dar es Salaam.
Inadaiwa, washtakiwa hao wakiwa watumishi wa CWT, walitumia madaraka yao vibaya na kujipatia Sh 13,930,963 kwa manufaa yao wenyewe.
Pia inadaiwa kuwa, katika tarehe na eneo hilo washtakiwa hao walichepusha kiasi hicho cha fedha mali ya CWT ,kwa kutumia nafasi walizokuwa nazo.
Hata hivyo, Washtakiwa wamekana kutenda makosa hayo na mshtakiwa Seif yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti yalitomtaka kuwasilisha mahakamani hapo fedha taslimu sh milioni 3.487,400 na kuwa mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya sh milioni saba huku Allawi akirudishwa rumande kw kushindwa kutimiza masharti hayo.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo umeshakamilika na hivyo wameomba tarehe ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali. Kesi imeahirishwa hadi Mei 17 kwa ajili ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali.
Home
MAHAKAMA
VIGOGO WAWILI CWT WAFIKISHWA MAHAKANI KUJIBU MASHTAKA YAO LIKIWEMO LA MATUMAMIZI MABAYA YA MADARAKA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...