Na Farida Mangube.
Vyombo
vya habari vya Mtandaoni na Waaandishi wa Habari Nchini WAMETAKIWA
kufuata misingi, kanuni, Sheria na maadili ya uandishi wa habari katika
kutekeleza majukumu ya kila siku ya kupashana habari mbalimbali, ili
kuondokana na mikanganyiko inayoweza kujitokeza baina ya vyombo vya
habari na Taasisi mbalimbali nchini.
Wito
huo umetolewa katika mafunzo ya Waandishi wa Habari za Mtandaoni
(Online Media) yalioandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadam
yenye lengo la kuwajengea uwezo wa namna ya kufanya kazi zao kwa weledi
kwa kufuata misingi ya Sheria ya Uandishi wa Habari
Akizungumza
katika Mafunzo hayo leo 10 Mei, 2021. Mratibu wa Taifa Mtandao huo
Onesmo Ole Ngurumwa amesema vyombo vya habari vya mtandaoni vinatakiwa
kufuata Sheria na kuacha kufanya Kazi kwa mazoea.
"Mafunzo
haya yanalenga kuwajengea uwezo vyombo vya Habari vya Mtandao, ili
muweze kufanya kazi zenu vizuri za kuhabarisha umma na unaposema
matumizi ya mtandao unazungumzia uhuru wa kujieleza" amesema Onesmo.
Aidha
ameongeza kuwa ni muhimu vyombo vya habari vya Mtandao vikasimama
vizuri na kuwa wanataaluma wazuri ambao watazingatia misingi, Sheria,
kanuni na taratibu za taaluma ya Uandishi wa Habari katika utaekelezaji
wa majukumu yao.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile
amewaomba THRDC kuviwezesha vyombo vya Habari vya Mtandao kuwa uchumi
unaotengamaa kwani vingi havina mipango ya biashara (Business Plan) huku
akiwasisitiza waandishi wa habari kuwa na hali ya kujijali wao wenyewe
wawapo kazini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...