KATIKA kuelekea sikukuu ya EID EL FITR Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kuimarisha ulinzi na usalama kwa kufanya misako na doria maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya na kupata mafanikio ikiwemo kukamata watuhumiwa wa makosa mbalimbali pamoja na mali za wizi.

KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].

Mnamo tarehe 12.05.2021 majira ya saa 11:30 asubuhi huko mtaa wa Iwambala, Kata ya Uyole, Tarafa ya Iyunga Jijini Mbeya. Tulimkamata ELIZABETH LEONARD [33] mkazi wa Iwambala akiwa na gongo ujazo wa lita 5.


KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].

Mnamo tarehe 12.05.2021 majira ya saa 20:15 usiku huko Kitongoji na Kijiji cha Mpanda, Kata ya Bondeni, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya. Tulimkamata JOHN BENARD [44] mkazi wa Ipinda akiwa na gongo ujazo wa lita 25.


KUPATIKANA NA MALI YA WIZI.

Mnamo tarehe 12.05.2021 majira ya saa 08:00 asubuhi huko eneo na Kata ya Nsalaga, Tarafa ya Iyunga Jijini Mbeya. Tulimkamata mhalifu sugu aitwaye YOHANA MFIRINGE [22] mkazi wa Nsalaga ambaye alikiri kufanya matukio 04 ya uvunjaji na wizi katika nyumba za watu. 

Katika upekuzi tuliofanya, tulimkuta na mali ya wizi ambazo ni:-

  1. Blanketi 13, 

  2. Redio Subwoofer 07 aina tofauti, 

  3. King’amuzi cha Star Times, 

  4. Spika 11, 

  5. Twiter spika 01, 

  6. Redio ndogo 03, 

  7. TV flat Screen aina ya TCL 01 inchi 32, 

  8. TV flat screen aina ya Sundar mbovu 01 inchi 32,

  9.  Sare ya JWTZ shati 01 na magodoro 02.


KUPATIKANA NA BIDHAA ZISIZO NA UBORA.

Mnamo tarehe 12.05.2021 majira ya saa 13:10 mchana huko mtaa wa Sabato, Kata ya Kyela Mjini, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya. Tuliwakamata NSAJIGWA LAZARO [42] na KELVIN OSWARD [28] wote wakazi wa Tukuyu – Rungwe wakiwa na pombe kali konyagi katoni 21 zidhaniwazo kuwa hazina ubora / kiwango wakitokea Dsm. 


KUPATIKANA NA BHANGI.

Mnamo tarehe 12.05.2021 majira ya saa 02:00 usiku huko eneo la Marafiki, Kata ya Ilomba, Tarafa ya Iyunga Jiji na Mkoa wa Mbeya. Tulimkamata MUSAKHARIM ISSA SALIM [24] Dereva wa Bodaboda na mkazi wa Sae akiwa na bhangi uzito wa gram 705 kwenye suruali aliyovaa.


KUKAMATA SILAHA NA RISASI.

Mnamo tarehe 12.05.2021 majira ya saa 09:00 asubuhi Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanikiwa kukamata silaha moja aina ya Shortgun, risasi 03 za Shortgun, mapanga matatu na shoka 01.

Tukio hili limetokea huko Kitongoji cha Igundu, Kata ya Sangambi, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya wakati watu wanaodhaniwa kuwa majambazi wakiwa katika harakati za kwenda kufanya uhalifu katika soko la dhahabu.

Kutokana na tukio hilo, Jeshi la Polisi linamshikilia mtu mmoja wakati mtu mmoja ambaye bado kufahamika jina lake aliuawa kwa kupigwa na wananchi waliojichukulia sheria mkononi akiwa katika harakati za kwenda kufanya uhalifu maeneo hayo ya masoko ya dhahabu.



Watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi wa mashauri yao kukamilika. Ninaendelea kutoa wito kwa watendaji wa Mitaa na Vitongoji kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kuwafichua wahalifu na kukemea vitendo vya uhalifu ikiwa ni Pamoja na kusuluhisha migogoro ya wananchi katika maeneo yao ili kuepuka madhara makubwa yasitokee. 


Imetolewa na:

[ULRICH O. MATEI- SACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...