* Kuwakutanisha na Serikali, mikakati ya kutoa huduma bora, uadilifu na nidhamu kujadiliwa
MKUTANO Mkuu wa nane wa kitaaluma wa Chama Cha Makatibu Muhtasi Tanzania umewakutanisha makatibu muhtasi nchini kote ambao wametoka Serikalini, mashirika ya Umma, taasisi zote za Serikali na ofisini za watu binafsi kwa siku mbili ambapo watajadili masuala mbalimbali ikiwemo mkakati wa kutoa huduma bora kwa uadilifu na nidhamu.
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Arusha leo kuhusiana na mkutano huo, Mwenyekiti wa TAPSEA Zuhura Songambele Maganga amesema, mkutano huo utafanyika katika kituo cha mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC,) na kueleza kuwa mkutano huo umefanyika kikatiba na unajadili kada inayohusu makatibu muhtasi.
"Katika mkutano huu wa siku mbili yaani tarehe 21 na 22, 2021 mada mbalimbali zitatolewa na wataalamu kutoka vyuo vyetu vya Serikali, na tarehe 21 mkutano wetu utafunguliwa rasmi na Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mh. Mohamed Mchengerwa na tunategemea uwepo wa makatibu wakuu kutoka Wizara hiyo bara na visiwani pamoja na viongozi kutoka TAMISEMI na wakuu wa vyuo vya utumishi kutoka bara na visiwani." Amesema.
Ameeleza kuwa, wamewaalika wakuu wa vyuo vya utumishi wa Umma kwa kuwa kada hiyo kama wadau watapata wasaa na kujadili masuala mbalimbali na kuyapatia Suluhu pamoja na kupeana fursa za kuboresha kada hiyo.
Aidha amesema, tarehe 22 kutakuwa na mkutano maalumu wa wanachama utakaojadili masuala mbalimbali yanayohusu wanachama wa kada hiyo.
"Mkutano huu unawashirikisha wanachama, tarehe 21 na 22 mkutano utawashirikisha makatibu muhtasi wote lakini mkutano wa tarehe 22 utawashirikisha wanachama na tutaweza kujadili kwa kina mapungufu, maelekezo, na hali halisi ya utendaji mzima wa kada hii." Amesema.
Aidha ameishukuru Serikali kwa kuanzisha shahada ya kada hiyo ambayo haikuwepo awali na hiyo imefanikiwa kutokana na mapendekezo yaliokuwa yanatolewa katika mkutano mkuu na 2017 mafunzo ya shahada ya Utumishi wa Umma yalianza kutolewa katika chuo cha utumishi wa Umma mkoani Dar es Salaam.
Vilevile ameipongeza Serikali na mashirika binafsi kwa kuona fursa hiyo na kuwaruhusu Makatibu Muhtasi kuhudhuria mkutano huu ambapo washiriki zaidi ya 100 wametoka Zanzibar na Pemba.
Mkutano huo wa nane wa chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania unakwenda na kauli mbiu ya "Kuwa Mbunifu Mahiri, Zingatia Weledi Katika Kuleta Mabadiliko ya Uchumi Tanzania." ambayo inawahimiza makatibu Muhtasi hao kwenda na wakati na kuweza kufanya kazi mahali popote ikiwemo katika Balozi mbalimbali.
Mwenyekiti wa TAPSEA Zuhura Songambele Maganga akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani ) leo jijini Arusha,kuhusu mambo yatakayojiri kwenye mkutano wao wa nane unaowakutanisha Makatibu Muhtasi zaidi ya 2000 kutoka mikoa mbalimbali nchini,katika mkutano huo wa Mwaka mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mh. Mohamed Mchengerwa

Mwenyekiti wa TAPSEA Zuhura Songambele Maganga (katikati) akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani ) leo jijini Arusha,kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya mkutano wao wa nane,unaotarajiwa kuzinduliwa kesho jijini humo,ambapo Makatibu Muhtasi zaidi ya 2000 tayari wamekwishawasili kushiriki mkutano huo wa Mwaka.Pichani kushoto ni Katibu wa TAPSEA Anneth Charles Mapima na kulia ni Dada Mwajuma.
Mkutano wa viongozi wa TPSEA na Wanahabari ukiendelea ukumbini.
Katibu wa TAPSEA akifafanua zaidi mambo mbalimbali ya mkutano huo ikiwemo na kueleza kauli mbiu yake kuwani 'kuwa mbunifu mahiri, zingatia weledi katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi Tanzania',na kuongeza kuwa Makatibu Muhtasi ni taswira ya ofisi kwani wamebeba majukumu makubwa ''hivyo tumeamua kuweka hii mikutano kila mwaka ili kuleta amsha amsha kwa makatibu Muhtasi katika kutenda kazi katika ofisi mbalimbali kwani wanahitaji kupata ujuzi mpya na maarifa mapya kila mwaka ili kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia katika nchi yetu,”alisema Bi Mapima.
MKUTANO Mkuu wa nane wa kitaaluma wa Chama Cha Makatibu Muhtasi Tanzania umewakutanisha makatibu muhtasi nchini kote ambao wametoka Serikalini, mashirika ya Umma, taasisi zote za Serikali na ofisini za watu binafsi kwa siku mbili ambapo watajadili masuala mbalimbali ikiwemo mkakati wa kutoa huduma bora kwa uadilifu na nidhamu.
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Arusha leo kuhusiana na mkutano huo, Mwenyekiti wa TAPSEA Zuhura Songambele Maganga amesema, mkutano huo utafanyika katika kituo cha mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC,) na kueleza kuwa mkutano huo umefanyika kikatiba na unajadili kada inayohusu makatibu muhtasi.
"Katika mkutano huu wa siku mbili yaani tarehe 21 na 22, 2021 mada mbalimbali zitatolewa na wataalamu kutoka vyuo vyetu vya Serikali, na tarehe 21 mkutano wetu utafunguliwa rasmi na Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mh. Mohamed Mchengerwa na tunategemea uwepo wa makatibu wakuu kutoka Wizara hiyo bara na visiwani pamoja na viongozi kutoka TAMISEMI na wakuu wa vyuo vya utumishi kutoka bara na visiwani." Amesema.
Ameeleza kuwa, wamewaalika wakuu wa vyuo vya utumishi wa Umma kwa kuwa kada hiyo kama wadau watapata wasaa na kujadili masuala mbalimbali na kuyapatia Suluhu pamoja na kupeana fursa za kuboresha kada hiyo.
Aidha amesema, tarehe 22 kutakuwa na mkutano maalumu wa wanachama utakaojadili masuala mbalimbali yanayohusu wanachama wa kada hiyo.
"Mkutano huu unawashirikisha wanachama, tarehe 21 na 22 mkutano utawashirikisha makatibu muhtasi wote lakini mkutano wa tarehe 22 utawashirikisha wanachama na tutaweza kujadili kwa kina mapungufu, maelekezo, na hali halisi ya utendaji mzima wa kada hii." Amesema.
Aidha ameishukuru Serikali kwa kuanzisha shahada ya kada hiyo ambayo haikuwepo awali na hiyo imefanikiwa kutokana na mapendekezo yaliokuwa yanatolewa katika mkutano mkuu na 2017 mafunzo ya shahada ya Utumishi wa Umma yalianza kutolewa katika chuo cha utumishi wa Umma mkoani Dar es Salaam.
Vilevile ameipongeza Serikali na mashirika binafsi kwa kuona fursa hiyo na kuwaruhusu Makatibu Muhtasi kuhudhuria mkutano huu ambapo washiriki zaidi ya 100 wametoka Zanzibar na Pemba.
Mkutano huo wa nane wa chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania unakwenda na kauli mbiu ya "Kuwa Mbunifu Mahiri, Zingatia Weledi Katika Kuleta Mabadiliko ya Uchumi Tanzania." ambayo inawahimiza makatibu Muhtasi hao kwenda na wakati na kuweza kufanya kazi mahali popote ikiwemo katika Balozi mbalimbali.
Mwenyekiti wa TAPSEA Zuhura Songambele Maganga (katikati) akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani ) leo jijini Arusha,kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya mkutano wao wa nane,unaotarajiwa kuzinduliwa kesho jijini humo,ambapo Makatibu Muhtasi zaidi ya 2000 tayari wamekwishawasili kushiriki mkutano huo wa Mwaka.Pichani kushoto ni Katibu wa TAPSEA Anneth Charles Mapima na kulia ni Dada Mwajuma.
Katibu wa TAPSEA akifafanua zaidi mambo mbalimbali ya mkutano huo ikiwemo na kueleza kauli mbiu yake kuwani 'kuwa mbunifu mahiri, zingatia weledi katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi Tanzania',na kuongeza kuwa Makatibu Muhtasi ni taswira ya ofisi kwani wamebeba majukumu makubwa ''hivyo tumeamua kuweka hii mikutano kila mwaka ili kuleta amsha amsha kwa makatibu Muhtasi katika kutenda kazi katika ofisi mbalimbali kwani wanahitaji kupata ujuzi mpya na maarifa mapya kila mwaka ili kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia katika nchi yetu,”alisema Bi Mapima.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...