Na Mwandishi Wetu
MSANII wa Muziki wa Kizazi Kipya Ali Kiba ameibua shangwe na nderemo katika kilele Cha onyesho la siku ya vibonzo lililoandaliwa na Clouds Media Groups linalofahamika kwa jina la clouds Mchongo.
Kilele cha onesho hilo kilifanyika kwenye uwanja wa michezo wa 'Business'uliopo Buza kwa Mama Kibonge.
Kiba aliibua shangwe hizo baada kupanda jukwaani na kuimba wimbo wake mpya wa 'Salute'.
Alipanda akiwa na kundi lake la madansa sambamba na mdogo wake Abdul Kiba na kuimba baadhi ya nyimbo zake ikiwemo wimbo wake mpya unaofahamika kwa jina la 'Salute,Ndombolo ya solo.
Wakongwe wengine ni Chegge Chigunda kutoka TMK amekonga nyoyo za watu huku akifuatiwa na mkongwe wa dansi Muumin Mwinjuma ambaye aliimba wimbo wake 'Kwa Mpalange' ambao ndiyo anatamba nao hivi kwa hivi sasa.
Kundi la watangazaji wa Kipindi cha Leo Tena kinachorushwa na kituo hiko kiliongoza jahazi la shughuli hiyo iliyodhaminiwa na DStv, majiko ya Moto Poa,Red Gold Tomato.
Aidha burudani zingine zilizojiri ni pamoja na kinyang'anyiro cha kumpata Miss Buza, pia wasanii mbalimbali ambao ni wazawa wa eneo hilo la Buza walipata nafasi ya kutoa burudani.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Ali Kiba pamoja wasanii wa Kundi lake la Kings Music Records wakitoa burudani katika kilele Cha onyesho la siku ya vibonzo lililoandaliwa na Clouds Media Groups linalofahamika kwa jina la clouds Mchongo
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Ali Kiba akitoa burudani ya nguvu katika kilele Cha onyesho la siku ya vibonzo lililoandaliwa na Clouds Media Groups linalofahamika kwa jina la clouds Mchongo
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Chege Chigunda akitoa burudani katika kilele Cha onyesho la siku ya vibonzo lililoandaliwa na Clouds Media Groups linalofahamika kwa jina la clouds Mchongo.
Mwanamuziki wa dansi, Muumini Mwinjuma akitoa burudani ya wimbo wa singeli uitwao kwa Mpalange katika kilele Cha onyesho la siku ya vibonzo lililoandaliwa na Clouds Media Groups linalofahamika kwa jina la clouds Mchongo.
Mtangazaji wa kipindi cha Leo Tena cha Clouds Fm Jose Mara akitoa salamu kwa mashabiki wao wakati wa kilele Cha onyesho la siku ya vibonzo lililoandaliwa na Clouds Media Groups linalofahamika kwa jina la Clouds Mchongo.
Mtangazaji wa redio ya Clouds Fm Gea Habibu akitoa salamu pamoja na kutambulisha kipindi chao kinachorushwa na radio hiyo wakati wa kilele Cha onyesho la siku ya vibonzo lililoandaliwa na Clouds Media Groups linalofahamika kwa jina la Clouds Mchongo
Wasanii mbalimbali wakitoa burudani
Msanii wa Maigizo, Bulton Mwemba ‘Mwijaku’ akiwa amembeba Miss Buza mara baada ya kutangaza kuwa Miss Buza wakati wa kilele Cha onyesho la siku ya vibonzo lililoandaliwa na Clouds Media Groups linalofahamika kwa jina la Clouds Mchongo
Mambo ya uswazi hayo
Baadhi ya wananchi walioudhuria kwenye kilele cha onyesho la siku ya vibonzo lililoandaliwa na Clouds Media Groups linalofahamika kwa jina la clouds Mchongo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...