Na Humphrey Shao, Michuzi TV


Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri Dennisi James leo amefanya ziara yake ya kwanza katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo shule , Hospitali,Kituo cha afya Kimara na Kituo cha mabasi cha Stendi ya Magufuli.

Akizungumza mara baada ya kukagua shule ya Msingi Makamba iliyopo Mbezi, Shule Sekondari Mashujaa Sinza amesema kuwa yeye kama mkuu wa Wilaya anaanza kazi hiyo katika Wilaya ya Ubungo kwa kutanguliza elimu kama kipaumebele chake cha Kwanza.

“Kipaumbele cha kwanza kwangu ni elimu lazima tuhakikishe kuwa wanafunzi wote wanapata nafasi ya kusoma vizuri mara baada ya kuchaguliwa kwani ni jambo la aibu kufika mwakani kusikia kwama tuna tatizo la madarasa na madawati kwenye shule zetu” amesema DC James.

Ametaja kuwa swala la kuandaa wanafunzi pakusomea sio jambo la ghafla kwani kila mratibu elimu anajua kuwa kuna wanafunzi wangapi wanamaliza katika shule za msingi zilizopo katika eneo lake hivyo ni vyema kujipanga kwa kuweka mipango mizuri kwa ajili ya sekondari zetu mwakani hili Watoto waweze kupata madarasa na madawati.

Akizungumza mara baada ya kukagua shule ya Msingi Makamba amesema kuna haja ya bodi ya shule hiyo kujitathmini juu ya mipango yao ya kuendeleza shule hiyo kuliko kusubiri ikama kutoka kwa mkurugenzi.

Alimaliza kwa kusisitiza kuwa kila mtu sasa anatakiwa kujipanga kuwa Ubungo inakuwa kipaumbele katika swala la elimu.  

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James akitoa Maelekezo kwa Watendaji na Maafisa waliopo katika Wilaya ya Ubungo Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo , Beatrice Dominic akizungumza jambo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kheri James wakati wa ukaguzi wa Miradi ya Maendeo



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...