KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM inatarajiwa kukutana Jumanne Juni 22, 2021 chini ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan.

Kikao hicho kimetanguliwa na kikao cha Secretariet ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika chini ya Mwenyekiti wake Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo kimefanyika katika ukumbi wa NEC White House Jijini Dodoma

"Ni kweli Jumanne 22 Juni 2021 Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ataongoza kikao cha kawaida cha kamati Kuu, maandalizi yote yamekamilika, ni kikao cha kawaida cha Kikatiba" Shaka Hamdu Shaka Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.
katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ndg Daniel Chongolo akizungumza wakati wa Kufungua kikao Cha Sekretarieti ya Halmashauri kuu ya CCM kilichofanyika katika Ukumbi wa makao makuu ya CCM White House jijini Dodoma Leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...