Mkuu
wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amezindua awamu ya pili ya
utengenezaji wa magari aina ya HONG YANG katika kiwanda cha GF
Assemblers Kibaha mkoni Pwani
Akizungumza baada ya uzinduzi wa
magari hayo, Kunenge alikemea baadhi ya tabia za watendaji wa serikali
za kupishana katika ofisi za wawekezaji kwa visingizio mbali mbali mbali
Ikiwamo
kulazimisha kuonana na wamiliki ama kwa visingizio vya kutaka kufanya
ukaguzi hali inayowafanya wawekezaji kuwa na hofu na kujikuta
wanashindwa kutimiza majukumu yao
Kunenge alisema Serikali ya
mkoa wa Pwani inahakikisha inapata maendeleo kwa kuongeza fursa ya
biashara na uwekezaji wenye mazingira rafiki na utawala bora kwa hiyo
hataki kusikia ama kuona watendaji wanakua kikwazo katika kufanikisha
mpango huo na kwamba hatawavumilia.
" wakati Serikali ikijenga
mazingira rafiki na wawekezaji sisi wenyewe mafisa wa Serikali tumekuwa
kikwazo , Nae Meneja wa kampuni GF Vehcle Assemblers , Ezra Mereng
alisema lengo lao ni kuunda kila aina ya chapa (brand ) ya magari kwa
kuwa teknolojia na mitambo waliyonayo inauwezo wa kuunganisha magari
aina zote zenye viwango na vigezo vya kitaifa na kimataifa.
Mereng
alisema kiwanda hicho kilianza kwa kuunda magari chapa aina ya FAW na
sasa wamezindua chapa ingine ya Hongyan na kuwataka wadau na
makampuni mengine ya magari kuacha kuagiza badala yake walete GFA
kuundiwa (Assembling) kwa zingatia vigezo vyoote vya kimataifa.
Mkuu wa mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge akipokea zawadi ya kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya GF Assemblers Imrani Karmali wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya utengenezaji wa gari jipya ya kubebea mizigo anina ya Hong Yang katika kiwanda hicho leo mkoani Pwani.Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akifurahia jambo na mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha GF Assemblers,Imrani Karmali baada ya uzinduzi wa awamu ya pili ya utengenezaji wa gari mpya ya kubebea mizigo aina ya Hong Yan katika kiwanda hicho mkoani Pwani
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...