Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo akifurahi jambo na Watu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) baada ya kutoka kwenye uapisho mkoani Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Fatma Almasi Nyagasa akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kutoka kwenye kiapo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla.

 Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Amos Makalla leo June 21, 2021 amewaapisha Wakuu wa Wilaya za Dar es Salaam baada ya kuteuliwa June 20, 2021 na Rais wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Wakuu wa Wilaya wapya walioapishwa na RC Makalla ni Fatma Almasi Nyangassa (Kigamboni) na Kherry Denis James (Ubungo) wakati Jokate Urban Mwegelo (Temeke), Godwin Crydon Gondwe (Kinondoni) Ng’wilabuza Ndatwa Ludigija (Ilala) wakiendelea na majukumu yao ya awali.

Baada ya uapisho huo, Makalla amewataka Wakuu hao kufanya kazi kwa bidii katika vituo vyao vya kazi walivyopangiwa na Mhe. Rais Samia Suluhu, amesema Rais anafahamu eneo kubwa la nchi ya Tanzania hivyo kuwa na imani nao katika nafasi hiyo ya uwakilishi wa Ukuu wa Wilaya.

“Nimefurahi kupata Wakuu wa Wilaya wapya, Kigamboni (Fatma Nyangasa) na Ubongo (Kherry James), naamini hawa wengine ni wazoefu katika majukumu yao hivyo natarajia mtafundishana kazi ili twende sawa”, amesema Makalla.

Amewataka Wakuu hao wa Wilaya kufika kwenye vituo vyao vya kazi na kutoa ushirikiano kwa Watendaji waliowatangulia katika vituo hivyo.

“Mkifika kwenye maeneo yenu ya kazi hakikisheni mnafanya kazi kwa bidii na ushirikiano, Rais amewaleta katika mkoa huu naamini ana matarajio na wote”, ameeleza Makalla.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya mpya ya Ubungo, Kherry James kwa niaba ya wenzake ameomba ushirikiano kwa sehemu walizopangiwa na Rais Samia Saluhu ili kufanikisha azma na matakwa ya Serikali ya Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...