Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imewaomba Viongozi wa Dini zote nchini kupitia Kamati za Amani za Mikoa yao kuangalia namna bora ya kujadili jinsi ya kudhibiti kelele na mitetemo ya sauti katika namna ya kulinda afya za waumini wao.

Pia imewataka wamiliki wa kumbi za starehe na nyumba za ibada kuhakikisha sauti zitokanazo na shughuli zao hazizidi viwango vilivyowekwa kisheria.

Akizungumza na Wandishi wa Habari jijini Dodoma leo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Selemani Jafo amesema kiwango cha sauti kwenye maeneo hayo ni 50 kwa muda wa mchana na 35 usiku.

Waziri Jafo ametoa wito kwa wamiliki wa kumbi za starehe na nyumba za ibada kuzingatia utaratibu wa kisheria na ambaye ataenda kinyume atachukuliwa hatua ikiwemo kifungo cha miezi sita au faini ya Sh Milioni Moja kwa ambao maeneo yao yataonekana kuleta athari za kelele.

" Nitoe wito kwa wamiliki wa maeneo haya kuzingatia utaratibu wa sheria uliowekwa, Katika kipindi cha Januari mpaka Machi mwaka huu, NEMC, ilipokea malalamiko 93 kutoka kanda mbalimbali ambapo Kanda ya Kati ilipokea malalamiko 30, Kanda ya Kaskazini (12), Kanda ya Ziwa (21), Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (6) na malalamiko 31 kutoka Kanda ya Mashariki.

Katika siku za karibuni malalamiko yamekua ni mengi dhidi ya wamiliki hawa hivyo nitoe wito kwa wahusika kuzingatia sheria, lengo la Serikali ni kulinda afya za wananchi wetu," Amesema Waziri Jafo.

Mkutano huo umehudhuriwa na Mawaziri mbalimbali akiwemo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Chilo, Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia, Omari Kipanga, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Walemavu, Ummy Ndairenanga na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Paulina Gekul.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Selemani Jafo akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...