Na Mbaraka Kambona,
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Prof. Erick Komba amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanafanya tafiti za kutosha ambazo matokeo yake yaweze kutumiwa na Wafugaji moja kwa moja na sio kufanya tafiti kwa ajili ya mambo ya sayansi tu.
Prof. Komba aliyasema hayo muda mfupi baada ya kumaliza kikao kazi cha kujadili mkataba wa utendaji kazi wa taasisi hiyo kilichofanyika katika makao makuu ya Ofisi hiyo iliyopo jijini Dodoma Juni 16, 2021.
Alisema kuwa lengo la taasisi hiyo ni kufanya tafiti na kueneza teknolojia ya tafiti hizo ili kuendelea kuboresha tasnia ya mifugo nchini.
"Sisi kama taasisi tumejikita katika kufanya tafiti za malisho na mbari za mifugo ili kuwafanya wafugaji waweze kufuga kwa tija na kunufaika na mifugo yao," alisema Prof. Komba
Aliongeza kuwa katika kipindi cha uongozi wake atahakikisha tafiti wanazozifanya zinaendelea kuwanufaisha Wafugaji na taifa kwa ujumla.
Aidha, Prof. Komba alitumia nafasi hiyo pia kuwahimiza Watendaji wa taasisi hiyo kufanyakazi kwa weledi, na kwa bidii ili waweze kuzalisha tafiti za kutosha na kuzisambaza kwa wafugaji ili waweze kuzitumia na kujiongezea kipato.
"Tangu nimeteuliwa kuongoza taasisi hii nina miezi miwili sasa, lakini mipango yangu ni kuhakikisha ninashirikiana kikamilifu na watafiti wenzangu ili tuweze kufanya tafiti zitakazoleta matokeo yatakayowasaidia wafugaji kupata tija na sio tafiti kwa ajili ya sayansi tu,"alifafanua Prof. Komba
Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya
TALIRI, Prof. Sebastian Chenyambuga alisema kuwa wajibu wa taasisi hiyo ni
kufanya tafiti na hivyo aliwataka watumishi
wahakikishe wanajipanga vizuri ili kazi zao ziwe na manufaa kwa wananchi
hususan wafugaji.Mtafiti Mkuu, Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI), Dkt. Jonas Kizima (katikati) akimuonesha Mwenyekiti wa Bodi ya TALIRI, Prof. Sebastian Chenyambuga (kulia) majani aina ya mikundekunde ambayo ni maalum kwa ajili ya kulishia mifugo yaliyopandwa katika eneo la Makao makuu ya Ofisi ya TALIRI iliyopo jijini Dodoma Juni 16, 2021. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI), Dkt. Daniel Komwihangilo.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI), Prof. Sebastian
Chenyambuga (kushoto) akimueleza jambo Mtafiti Mkuu, TALIRI, Dkt. Jonas
Kizima (katikati) alipokuwa akikagua mbegu ya majani ya Juncao
iliyopandwa kwenye Kitalu kilichopo katika eneo la Ofisi ya taasisi
hiyo. Mwenyekiti huyo alifika katika makao makuu ya taasisi hiyo jijini
Dodoma Juni 16, 2021 ambapo pamoja na mambo mengine aliwasisitiza
watumishi wa Taasisi hiyo kufanya kazi kwa bidii na kwa Weledi ili
kuongeza tija katika kazi zao za kila siku.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...