Afisa Maendeleo wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam Humphrey Jimmy akitoa elimu ya usafi wa Mazingira kwa Wananchi wa Mtaa wa Jitegemee Mabibo ambapo utawanufaisha nyumba 250 na kujenga vyoo vya umma ndani ya Halmashauri zote za Dar es Salaam.
Mtaalamu wa masuala ya Jamii Byera Mutabazi kutoka kwa Wahandishi Washauri MS DOHWA akielezea umuhimu wa wananchi kunufaika na mradi huo utakaoondoa changamoto ya usafi wa mazingira ndani ya Jiji la Dar es Salaam.
Afisa Mawasiliano na Jamii wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA Elizabeth Eusebius akitoa elimu ya usafi wa mazingira kwa wananchi wa Mtaa wa Jitegemee Kata ya Mabibo utakaoondoa changamoto ya majitaka na usafi wa mazingira ndani ya Jiji la Dar es Salaam.
Wananchi wa Mtaa wa Jitegemee Kata ya Mabibo wakisikiliza mkutano  ulioandaliwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam(DAWASA) kuhusu uboreshaji wa huduma ya usafi wa mazingira.

Na Zainab Nyamka, Michuzi TV
MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kujenga vyoo vya umma 30 katika maeneo tofauti ndani ya Jiji la Dar es Salaam ili kuboresha usafi wa mazingira.

Vyoo hivyo vitajengwa katika maeneo yenye mkusanyiko wa watu ikiwemo masoko na vituo vya mabasi ndani ya Halmashauri zote.

Pia,Nyumba 250 zinatarajia kunufaika na mradi wa ujenzi wa vyoo vitakavyowekewa mfumo wa kutiririsha majitaka kuelekea kwenye mabwawa kwa eneo la Mtaa wa Jitegemee Mabibo.

Wakizungumza na wananchi wa mtaa wa Jitegemee Mabibo, Afisa Maendeleo DAWASA Afisa Maendeleo Humphrey Jimmy amesema miradi hii itaenda kusaidia kutatua changamoto za usafi wa mazingira baada kupata mkopo kutoka Benki ya Dunia na utasimamiwa na Dawasa.

Amesema, kutokana na watu kutokuwa na mifumo mizuri ya kuhifadhi majitaka maeneo mengi hukumbwa na magonjwa wa mlipuko na hivyo Wamewataka wananchi wa eneo la Mabibo kupokea miradi mikubwa ya majitaka ili kuboresha usafi wa mazingira.

“Dawasa imeweka mpango wa kuboresha huduma zake za usafi wa mazingira katika maeneo yenye makazi yasiyo rasmi na kukosa mpangilio, makazi yenye msongamano wa nyumba , kipato cha chini na maeneo yaliyo nje ya mfumo wa mtandao wa ukusanyaji majitaka,”amesema Jimmy

“Maeneo mengine ni yale yenye uwezekano wa kuwa na mlipuko wa magonjwa yanayosababishwa na maji na pia Dawasa watapeleka mradi huo kwa jamii itakayokubali na yenye huhitaji na iko tayari kupokea huduma hiyo.” Amesema.

Jimmy amesema, Katika kupunguza na kutatua changamoto na matatizo ya usafi wa mazingira Dawasa imeweza kuchagua maeneo kwa ajili ya mradi kwa kuboresha huduma ya ukusanyaji majitaka kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo Mabibo.

Kwa upande wa Wahandisi washauri wa Mradi huo, MS DOHWA, Mtaalamu wa Masuala ya Jamii Byera Mutabazi amesema jumla ya nyumba 250 zitanufaika na mradi huo wa utoaji wa majitaka majumbani ambao utasaidia kutatua changamoto ya majitaka katika eneo la Mabibo.

“Uboreshaji wa usafi wa mazingira utahusisha ujenzi wa vyoo vya Jumuiya kwenye maeneo ya masoko na vituo vya mabasi, ujenzi wa mitandao ya mifumo ya ukusanyaji majitaka kutoka majumbani, ujenzi wa mitambo ya kuchakata majitaka yatokayo majumbani na sehemu ya kuhifadhi majitaka,”amesema Mutabazi.

Amesema vyoo vitakavyojengwa kwa wananchi vitakuwa vinatiririsha maji hadi katika bwawa la majitaka na wamewataka kutokutupa taka ngumu ili wasizibe mfumo huo.

Wananchi wa Mabibo wameomba mradi huo uwafikie wote wenye uhitaji ili kuweza kupata huduma hiyo muhimu kutoka Dawasa.

Miradi ya majitaka imeendelea kutekelezwa kwa kasi ndani ya Jiji la Dar es salaam katika maeneo tofauti kwa kujenga mabwawa makubwa ya kupokea majitaka na mifumo ya kuchataka maji taka ili kuboresha usafi wa mazingira.

Katika uboreshaji mradi wa vyoo kwa wananchi kwa kujenga hadi hatua ya msingi na Mwananchi atatakiwa kumalizia na kuezeka choo chake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...