
Mwenyekiti wa Bodi ya VETA Dk.Peter Maduki akipata maelezo kutoka kwa Meneja Uhusiano wa VETA Sitta Peter kuhusiana na kozi mbalimbali zinazotolewa na Vyuo vya ufundi stadi wakati Mwenyekiti huyo alipotembelea banda VETA katika maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
*VETA yawa mchango katika Sekta ya Viwanda kwa uzalishaji es Rasilimali yenye ujuzi.
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imesema taaluma ya Ufundi Stadi inaendelea kukua kila siku kwa sababu kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali katika jamii.
Changamoto zilizo katika jamii kushindwa kupata ufanisi ni Sekta ya Kilimo,Ufugaji, Usindikaji wa vyakula, Sekta ya viwanda kwa ajili ya Rasilimali Watu wenye ujuzi.
Licha ya kuwa na mafanikio hayo VETA inahitaji kupata Walimu ambao watawezesha mafunzo kuendelea kwa baadhi ya Walimu wanastaafu.
Akizungumza jana katika Maonesho ya 45 Biashara yl Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Sabasaba Mwenyekiti wa bodi ya VETA Dkt Peter Maduki amesema Mamlaka yao inakwenda na wakati na ndio maana wanafanya kazi zao kwa timu kwa kufanya utafiti dhidi ya changamoto zinazoizunguka jamii.
Maduki amesema,katika kipindi hiki cha maonesho ya 45 wamejipanga kuonesha bunifu mbalimbali ikiwemo,maabara inayotembea ambayo itaondoa changamoto kubwa katika shule ambazo hazina maabara.
"Tumejipanga kuongeza uchumi katika sekta ya viwanda hasa kwa vijana wanaonza vyuo na hata waliopo kazini tayari,"alisema Maduki.
Alisema hata wafanyakazi waliopo kazini kwa muda mrefu wanatakiwa wafike VETA kwa ajili ya kupata mafunzo mbalimbali ili kuongeza tija katika kazi yake.
Naye,Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dk.Pancras Bujulu alisema katika maonesho ya mwaka huu wamejipanga kuonesha bidhaa za mikakati ikiwemo,vifaa vya kilimo,viwanda na ufugaji.
Alisema hivi sasa VETA imejiimarisha zaidi katika utoaji wa elimu kwa kuongeza vyuo 33 katika mikoa mbalimbali nchini na kufanya kuwa na jumla ya vyuo 71.
"Tanzania ni moja ya nchi inayoendelea katika mapinduzi ya viwanda hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kuanzisha vyuo vya Sayansi na Teknolojia ili wanafunzi wajue zaidi masuala ya ubunifu ambayo yanakwenda sambasamba na uchumi wa viwanda,"alisema Dk.Bujulu.
Dk.Bujulu amesema bunifu zao zinaongeza ufanisi zaidi katika jitihada za uchumi wa viwanda.
Mwenyekiti wa Bodi ya VETA Dk.Peter Maduki (mwenye suti nyeusi)akipata maelezo kutoka kwa Mwalimu wa Chuo cha VETA Chang'ombe Kintu Kilanga ambaye anaofundisha vijana wenye mahitaji maalum wakati alipotembelea banda VETA katika maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya VETA Dk.Peter Maduki (mwenye suti nyeusi) akipata maelezo kutoka kwa Mwalimu chuo cha Udereva VETA Kihonda mkoani Morogoro William Munuo wakati Mwenyekiti wa Bodi hiyo alipotembelea banda VETA katika maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam. kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dkt. Pancras Bujulu
Mwenyekiti wa Bodi ya VETA Dk.Peter Maduki akipata maelezo kutoka kwa Mwalimu wa Chuo cha Ualimiu wa Ufundi Stadi Morogoro Sophia Tukka wakati alipotembelea banda VETA katika maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Picha mbalimbali za Mwenyekiti wa Bodi wa VETA Dk.Peter Maduki na Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dk. Pancras Bujulu wakitembelea Banda la VETA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...