“Nafurahia zaidi uhuru ninaopata kufanya kazi kupitia mfumo wa Bolt. Nina uhuru wa kufanya kazi masaa ninayotaka na wakati ninaotaka. Nilianza udereva na Bolt nilipokuwa nasoma chuo, na shughuli hii imeniwezesha kujikimu kimaisha. Nimeweka akiba ya hela kwa mipango ya kuanzisha biashara ya duka la vifaa vya ujenzi nikishirikiana na marafiki zangu.


Mfumo wa usafiri kupitia mtandao ni nafuu na abiria wanaweza kusafiri kwa raha bila kumiliki usafiri binafsi.

Ninashauri vijana leo kuwa na ujasiri na wasiogope kuanza na kujaribu vitu vipya ambavyo vinaweza kuwainua kimaisha. Ninajivunia kile nilichofanikiwa mpaka sasa. Nilianza kuendesha gari kwa mkataba na kampuni na niliweza kuweka akiba ya kutosha kununua gari langu mwenyewe. Mfumo wa usafiri wa mtandao kupitia Bolt umechangia sehemu kubwa katika mafanikio yangu ” – Dereva Bolt, Jeremiah Laurence Salufu (27), Salasala – Dar es Salaam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...