Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango amehudhuria ufunguzi wa Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa (Generation Equality Forum) linalofanyika Paris Ufaransa. Makamu wa Rais anamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika Jukwaa hilo.

Jukwaa hilo lenye madhumuni ya kuchagiza Usawa wa kijinsia linajadili Umuhimu wa uwezeshaji wanawake kiuchumi kama nyenzo ya kumnyanyua mwanamke kwa maendeleo na ustawi wa jamii. Kati ya mambo yaliyojadiliwa katika jukwaa hilo ni kumwezesha mwanamke kupata Teknolojia rahisi na sahihi katika kufanya shughuli za kiuchumi; kutolewa mafunzo ya ujasiriamali pamoja na utoaji wa mitaji kwa wanawake pamoja uwepo wa mifumo sahihi ya kidigitali katika shughuli za kiuchumi zinazofanywa na wanawake.

Katika Jukwaa hilo hii leo Julai 1 ,2021 Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango anatarajia kutoa Ahadi za Tanzania kama kinara wa uwezeshaji wanawake kiuchumi kama ilivyoridhiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango Akifuatilia Mada mbalimbali zinazowasilishwa katika Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa ( Generation Equality Forum)  Paris – Ufaransa.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akifurahia jambo na Rais wa Kenya Uhuru kenyata Mara baada ya kuwasili katika Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa ( Generation Equality Forum) Paris – Ufaransa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...