
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na aliyekuwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Nanyumbu Hamis Dambaya mara baada ya kukagua majengo ya stendi ya mabasi ya Mangaka. Makamu wa Rais aliagiza kusimamishwa kwa Mkurugenzi huyo ili kupisha uchunguzi kufuatia matumizi mabaya ya fedha za mradi huo.PICHA – OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiwasili kati ya JIda kuweka jiwe la msingi Soko la wafanyabiashara ndogondogo la Jida lililopo Wilaya ya Masasi. Soko hilo linagharimu Silingi milioni 619.9.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akipokea maelezo kutoka kwa Leonard Mkondola ambaye ni Fundi mchundo wa soko la kisasa la Jida mara baada ya kuwasili kuweka jiwe la msingi sokoni hapo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na wananchi waliojitokeza kumsikiliza wakati alipofika kuweka jiwe la msingi katika soko la kisasa la Jida lililopo Wilaya ya Masasi.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...