Mhitimu wa Chuo cha Ufundi VETA Chang'ombe mkaoni Dar es Salaam akifafanua jambo kwenye maonesho hayo.
Rechel Miyovela ambaye ni Mhitimu wa VETA Chang'ombe akikamua mafuta kwa kutumia mashine maalum ambayo wameibuni kwa kushirikiana na VETA Chang'ombe.


Na Said Mwishehe, Michuzi TV

VIJANA ambao wako mtaani baada ya kumaliza elimu ya msingi au sekondari wameshauri kujiunga na Chuo cha Ufundi(VETA) ili kupata ujuzi ambao unaweza kuwasaidia katika maisha yao kwa kubuni mashine na mitambo inayoweza kutumika katika shughuli za uzalishaji mali , hivyo kujipatia kipato.

Akizungumza na Michuzi TV na Michuzi Blog kwenye Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere mkoani Dar es Salaam , Mhitimu wa Chuo cha VETA Chang'ombe Rechel Miyovela amesema yeye ni miongoni mwa wahitimu wa chuo hicho ambaye leo ananufaka na elimu ya ujuzi ambayo ameipata na sasa amebuni mashine ya kukamua mafuta.

Mhitimu huyo ambaye yuko kwenye Banda la VETA, amesema katika maonesho hayo wamepeleka mashine ambazo zinatumika kukamua mafuta ya alizeti, karanga, korosho, na ubunifu huo ni matokeo ya uwepo wa VETA kwan wamejifunza mambo mengi na leo yamekuwa msaada kwao.

"VETA tunafunza vitu mbalimbali ambavyo vyenyewe vinatusaidia, kama wahitimu tukishaenda mtaani tunaweza kujiajiri na kufanya shughuli zetu wenyewe bila kutegemea mtu mwingine.Mtu akitoka VETA anaweza kufanya mambo yake mwenyewe ikiwemo kubuni mashine au mitambo kama sisi tulivyobuni mashine za kutengeneza mafuta.

"Kwa kutumia mashine hizi tunakamua mafuta na kisha yanatumika kama dawa inayoweza kuondoa mba kichwani, fangasi  wa miguu na sehemu za siri,michirizi kwa wanawake na mafuta haya ni kinga dhidi ya U.T.I.Nawashauri vijana walioko mtaani kujiunga na VETA ili kupata ujuzi wa aina mbalimbali .

"Mitambo yetu kwa anayehitaji anaweza kufika VETA Chang'ombe kwani licha ya kwamba tumehitimu bado tuko VETA na tunashirikiana na VETA Chang'ombe kutengeneza hizi mashine,"amesema na kuongeza kuna vijana wengi wakimaliza darasa la saba wanaona hawana nafasi ya kujiendeleza.

Hivyo ametoa mwito kwa vijana hata wakiwa na elimu ya darasa la saba au sekondari ni vema badala ya kukaa mtaani wakajiunga na VETA ili kwenda kupata kozi mbalimbali na wakitoka hapo watakuwa sehemu ya watu ambao wamepata ujuzi utakaowasaidia katika maisha yao.

Amesema VETA wanafundisha kozi nyingi na mtu akihitimu katika chuo hicho anaweza kufanya mambo makubwa kuliko hata mtu mwenye elimu kubwa. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...