Naibu Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul amezisisitiza Taasisi mbalimbali nchini kutoa nafasi kwa Watumishi wao kushiriki katika michezo ili kuimarisha afya zao.

Naibu Waziri Gekul amesema hayo Juni 30, 2021 Jijini Dodoma alipokuwa mgeni rasmi katika fainali za Mshindano ya Mpira wa Netiboli kwa Mkoa wa Dodoma yaliyoandaliwa na Chama cha Netiboli mkoani humo.

“Watumishi wakishiriki katika michezo  itawajengea afya, urafiki, ushirikiano, amani, upendo na  furaha pia, jambo hili ni kubwa kwa kuwa litawajengea mazingira  wafanyakazi hao kutumikia vizuri majukumu yao”, amesema Naibu Waziri Gekul.

Aidha Naibu Waziri Gekul amesema kupitia Bajeti ya Mwaka 2021/ 2022 tayari kuna mkakati wa kuanzishwa kwa Mfuko wa Michezo ambapo fedha zitakazopatikana zitatumika kutatua changamoto zinazokabili uendeshaji wa michezo  ikiwemo mchezo wa Netiboli.

Awali katika risala ya chama hicho  zimetajwa changamoto kadhaa ikiwemo uhaba wa fedha za Chama hicho kujiendesha, kukosekana kwa ofisi rasmi za chama na pia ukosefu wa viwanja vya mchezo wa Netiboli kwa Mkoa wa Dodoma ambazo Serikali imezipokea na kuonesha dhamira ya kuzishughulikia.

Katika mashindano hayo Timu ya TAMISEMI Dodoma imeibuka mshindi wa kwanza huku nafasi ya pili ikishikwa na timu ya Kongwa DC na nafasi ya tatu ikichukuliwa na Ihumwa Dodoma.

Mashindano hayo yamejumuisha jumla ya timu kumi ambazo ni TAMISEMI (Dodoma), Kongwa DC, Vijana (Dodoma), Ihumwa (Dodoma), Benjamin Mkapa Hospitali (Dodoma), Chuo Kikuu cha Kampala (Dar es Salaam), Wazalendo (Wanawake, Zanzibar), Wazalendo (Wanaume, Zanzibar), Muungano (Dodoma) na Bright (Dodoma).





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...